Uncategorized

Serikali Kubadili Kikosi cha Wanyamapori Kuwa Jeshi Kamili

Na. Zahara Musa

Serikali ya Tanzania imeandaa mabadiliko makubwa ambayo yanalenga kubadilisha Kikosi cha Wanyamapori nchini kuwa Jeshi Kamili la Kusimamia Hifadhi na Mbuga nchini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Jumanne Maghembe alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV wiki iliyopita.

Katika kukabiliana na mbinu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa kufanya uhalifu katika mbuga za wanyama amesema kuanzia mwezi wa kumi na moja mwaka huu kutakuwa kumeanzishwa jeshi kamili kwaajili ya wanyama pori tofauti na ilivyosasa walinzi hawatambuliki kisheria amesema Waziri Maghembe.

Wakati huo huo, Waziri huyo amesema kuwa Serikali inafanya mazungumzo na umoja wa mataifa na nchi ambazo ni wanunuzi wa pembe za ndovu ili kumaliza biashara hiyo duniani na kuwanusuru tembo wachache waliobaki nchini.

Waziri Mghembe amesema kuwa hatua hiyo ya serikali ni katika jitihada za Kunusuru tembo ambao wanaendelea kuuwawa kwakasi kubwa kutokana na pembe zake kununuliwa kwa bei kubwa.

Ameelezea kuwa serikali imejizatiti katika kukabiliana na majangili nchini hasa ukizingati kuwa na wao hutumia mbinu mpya kila mara katika kutekeleza azima yao ambapo zimenunuliwa ndege kumi na tano ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na majangili.

Amesema kuwa wanyama hao ambao ni kivutio kikubwa kwa watalii wameendelea kupungua siku hadi siku kutokana na kuuwawa kwa kasi ambapo wametoka kiasi cha laki tatu mwaka 1962 na kufikia tembo elfu arobaini na tatu hivi sasa.

Aidha ameonesha kusikitishwa na kitendo cha afisa mmoja wa wanyamapori ambaye alishirikiana na majangili yaliyoangusha ndege ya doria mwashoni mwa mwaka jana na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo rubani wa ndege hiyo amesema hawatosita kuwachukulia hatua kali za kisheria mfanyakazi yoyote atakaye jihusisha na uhalifu huo

Akielezea utalii kwa ujumla waziri Mghembe amesema kuwa, utalii ni sekta ambayo inaliingizia taifa pato kubwa la bilioni 22.2 kwa mwaka kupitia kwa watalii milioni moja na laki mbili wanaotembelea vivutio mbalimbali nakueleza kuwa serikali imeendelea kutangaza Duniani na baada ya miaka mitano ijayo matarajio ni kupata watalii milioni tatu ambao wataongeza pato hilo hadi kufikia bilioni tano kwa mwaka.

Amesema kuwa jitihada moja wapo ambayo imefanywa na serikali katika kutangaza utalii ulipo nchini ni pamoja na kuutangaza kwa kutumia televisheni ya ABC ambayo mwezi machi mwaka huu ilitangaza vipindi vyake moja kwa moja kutoka katika mbuga ya Ngorongoro.

Waziri huyo amesema kuwa vipindi hivyo vya ABC vimeangaliwa na watazamaji milioni kumi Duniani Kwote na hivyo itasaidia kuongeza idadi ya watalii wanakuja nchini, pia hutangaza kwa kupitia majarida mbalimbali likiwemo jarida la Safari.

Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa wingi wa vivutio ikiwa nyuma ya nchi ya Brazil na inashika namba moja katika bara la Afrika ambapo utalii huliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia ishirini na tano.

(7)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available