Uncategorized

Meli za Kijeshi za Iran Zatia Nanga Dar

Meli za Kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu zimetia nanga katika bandari ya Dar-es-Salaam, Tanzania katika ziara ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki baina ya Tanzania na Iran. Meli hizo tatu za Shaheed Naqdi (Pichani), Lavan na Bushehr zimetia nanga Jumanne hii zikiwa katika sehemu ya mafunzo ya jeshi la Baharini la nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Balozi wa Iran nchini Tanzania Bw. Mehdi A’qa Jafari amesema kuwa ziara hiyo inalengo la kutuma ujumbe wa amani kwa nchi za Afrika ya Mashariki na hasa kwa Tanzania nchi ambayo imekuwa na uhusiano wa kihistoria na Tanzania. Ziara hiyo ya siku nne itaendeleza urafiki kati ya nchi hizi mbili kwa mujibu wa Balozi huyo.

Pamoja na kuendeleza uhusiano mwema uwepo wa vikosi vya Baharini vya Iran katika eneo la Bahari ya Hindi umesaidia pia kuendeleza hali ya utulivu na usalama kwa vyombo vinavyosafiri eneo hili. “Uhusiano wa karibu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Kiafrika unanafasi ya pekee katika kudumisha amani na usalama na kulinda vyombo vya habarini katika eneo hili” alisema Balozi Jafari.

Maafisa wa Irani wanatarajia kufanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jeshi la Tanzania na kukutana na maafisa wenzao kutoka JWTZ kabla ya kurejea Iran.

Mwandishi ZM

(13)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available