Habari Kuu SAYANSI & TEKNOLOJIA Uncategorized

Magufuli Azindua Daraja la Kigamboni; Dk. Dau Azungumza

Magufuli akiwa na Dk Dau wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni. Picha na Ikulu

Na. Zahara Mussa

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. John Pombe Magufuli jana amezindua daraja la kisasa lenye kupita juu ya bahari na kuunganisha eneo la Kigamboni na Kurasini na hivyo kuondoa ulazima wa kupanda ferry au kufanya mzunguko mkubwa kuelekea Kigamboni. Zoezi hilo la ufunguzi lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar-es-Salaam, wahandisi na wadau wakuu wa mradi huo.

Daraja hilo la Kigamboni lina urefu wa mita 680 na likia na njia sita – tatu  kila upande likishikiliwa uzito wake kwa kiasi kikubwa na nyaya pamoja na milingoti ya saruji.

Rais aliwataka Watanzania waamini kuwa daraja hilo lililoanza kujengwa mwaka 2014  limetumia kiasi cha shilingi bilioni 254 kutokana na ugumu uliokuwepo wakati wa ujenzi na kuachana na fikra za kuibiwa hata sehemu ambayo hakuna tukio la aina hiyo.

Naye Balozi Dau akiongea baada ya kupewa nafasi ya upendeleo alimshukuru rais kwa kujali utendaji wake na kuzitaka taasisi nyingine za mfuko ya hifadhi ya jamii zijifunze kupitia (NSSF) kwa kuwaletea wananchi maendeleo, kukuza pato la Taifa kwa kuweka ushindani wenye tija.

Hatua hii ya rais Magufuli kumpatia nafasi aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF wakawi wote tangu mradi huu kuanza hadi alipombadilisha nafasi yake miezi michache nyuma imeonekana ni ishara ya imani yake kwake kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa NSSF. Wiki chache zilizopita kumekuwa na tuhuma mbalimbali dhidi ya uongozi wa Dk. Dau akiwa NSSF kiasi kwamba baadhi ya magazeti na mitandao ya jamii imejadili sana suala la uadilifu wake.

Kitendo cha Rais Magufuli kimetafsiriwa kuwa ni kumdhihirisha mbele ya jamii Balozi Dau kuwa hausiani na kashfa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo vya habari zikimtuhumu kutumia vibaya nafasi yake ya ukurugenzi (NSSF) kwa kujilimbikizia fedha.

Aidha rais Magufuli alivitaka vyombo vya habari kuwa na uzalendo wakati wa kuropoti habari ambazo zitaleta tija na maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa anashangazwa na vyombo vya habari kushindwa kuweka uzalendo wakati wa kuripoti mambo yanayolihusu taifa kwa kuyapa kipaumbele kitendo ambacho kinasababisha nchi jirani kutangaza mambo mazuri yaliyopo Tanzania yako kwao.

Daraja hilo  limejengwa kwa ushikiano wa (NSSF) iliyotoa asilimia 60 na serikali imetoa asilimia 40  ambapo jumla ya watanzania 300 watapata ajira na Kutakuwa na ofisi za Zima moto, polisi, utawala, na maabara katika eneo hilo. Mradi mzima unafuata mfumo wa taasisi binafsi kujenga na baadaye kurudis

(7)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available