Habari Kuu Uncategorized

Magufuli Amtimua Kitwanga

Charles Kitwanga

Na. M. M. Mwanakijiji

Katika kile kinachoonekana kuwanyamazisha wakosoaji wake wengi Rais John P. Magufuli amemfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Charles Kitwanga kwa kile ambacho taarifa ya Ikulu imekisema kuwa ni “kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia Bungeni na kujibu swali linaloihusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa”. Taarifa hiyo ya Ikulu ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu  Bw. Gerson Msigwa.

Kabla ya kuachishwa kazi Bw. Kitwanga alitajwa kuwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusika na kilichotajwa kuwa ni kashfa ya Lugumi ambapo Waziri huyo alihusishwa na mkataba wa mfanyabiashara Said Lugumi ambapo alipatiwa tenda na Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo baadaye Kitwanga alikuja kuingoza.

Katika taarifa ya jana usiku wa Ijumaa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuthibitisha tukio hilo Waziri Mkuu Bw. Kassim Majaliwa amesema kuwa kuna sheria za utumishi wa umma zinazomkataza mtumishi wa umma kwenda kazini akiwa amelewa.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi” ilisema taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Bw. Kitwanga anakuwa ni waziri wa kwanza katika serikali ya Magufuli kufukuzwa kazi na hivyo kuthibitisha kuwa msemo wa “hapa kazi tu” ambao Rais Magufuli amekuwa akiutumia tangu wakati wa kampeni hadi hivi sasa anaumaanisha kweli na hivyo wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa ni kutuma ujumbe wa wazi kwa watumishi wengine (wakiwemo mawaziri) kuwa hakuna tabia yoyote ambayo inaweza ikamfanya mtumishi kuonekana kushindwa kazi ambayo itavumuliwa.

(4)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available