NZITO ILIYOINGIA Uncategorized

Licha ya Wapinzani Kususa; Shein Ashinda Uchaguzi wa Marudio Zanzibar

Mwandishi Wetu – Zanzibar

Dk. Ali Mohammed Shein ameshinda uchaguzi wa marudio wa Urais na Wawakilishi huko Zanzibar kwa kushinda kwa asilimia 91.4 ya kura zote zilizopigwa. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha amemtangaza Shein kuwa mshindi wa uchaguzi huo licha ya chama kikuu cha upinzani na mgombea wake Maalim Seif Sharrif Hamad kususia uchaguzi huo na hivyo kutoa njia nyeupe kwa ushindi wa CCM na mgombea wake.

seifsharif
Seif Sharif Hamad

Wananchi wa Zanzibar jana walijitokeza kwenda kupiga kura katika uchaguzi  wa marudio wa kuchagua Rais, Wawakilishi na Mbunge wa Jimbo la Kijitoupele. Uchaguzi huu umerudiwa baada ya matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kufutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufuatia kile kilichoitwa hitilafu kubwa ambazo ziliondoa kuaminika kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Marudio ya Uchaguzi huo jana yalikubaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku chama kikuu cha Upinzani visiwani humo cha Chama cha Wananchi (CUF) kikisusia uchaguzi huo. Vyama vingine vidogo vya upinzani humo vingine viliamua kushiriki na vingine vikiungana na chama cha CUF kususia uchaguzi huo.

Pamoja na kususia huko bado wananchi wa visiwa hivyo walijitokeza japo si kwa wingi kama ilivyokuwa Oktoba na kwenda kupiga kura katika hali ya utulivu mkubwa kuliko ilivyotarajiwa.

hamadrashid
Hamad Rashid

Matokeo ya uchaguzi huo hata hivyo yanaonesha kuwa idadi kubwa ya Wazanzibar waliamua kuharibu kura zao kama namna ya kupinga marudio ya uchaguzi huo. Kura zilizoharibika zilikuwa 13,538 wakati kura za chama cha upinzani cha ADC ambacho mgombea wake Hamad Rashid Mohammed aliwahi kuwa kiongozi wa CUF kabla ya kuvuliwa uanachama alipata kura 9734 wakati yule wa CUF ambaye chama chake kilitangaza kujitoa kwenye uchaguzi huu wa marudio alipata kura 6076.

Kwa mujibu wa Jecha Dk. Shein amepata kura 299,982 kati ya kura 341,485 ya kura zote zilizopigwa. Idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 503,580.

(6)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available