Habari Kuu NZITO ILIYOINGIA Uncategorized

Dkt. Godius Kahyarara Mkurugenzi Mpya NSSF; TBC na RAHCO Wapata Wakurugenzi Pia

Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF) kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ramadhan Dau ambaye aliteuliwa na Rais kuwa Balozi. Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Ikulu Gerson Msigwa, “Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.”

Pamoja na uteuzi huo Rais Magufuli amemteua pia Dk. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi mpya wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) huku naye akijaza nafasi iliyoachwa na Clement Mshana ambaye amestaafu.

Pamoja na teuzi hizo mbili Rais pia amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hodhi ya raslimali za Reli Tanzania (RAHCO) ambaye anachukua nafasi ya Benhard Tito ambaye alifukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo teuzi hizo zote tatu zinaanza mara moja.

kahyararaHata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na Ikulu haikuweka bayana wateuliwa hao watatu walikuwa na nafasi gani kabla ya teuzi zao leo. Hata hivyo uchunguzi wa Zama Mpya unaonesha kuwa Prof. Kahyarara alikuwa ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Dr. Kahyarara alisoma elimu ya Sekondari Tambaza na baadaye Mazengo kwa elimu ya kidato cha tano na cha sita na baadaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam mwaka 1989 ambako alisoma Uchumi kwa shahada ya kwanza na kuunganisha shahada ya Uzamili hapo hapo chuoni.

ayubrioba
Ayub Rioba

Dkt Ayub Rioba ni mwandishi wa muda mrefu wa makala na habari mbalimbali nchini ambaye si mgeni miongoni mwa waandishi wa habari. Amekuwa akiandikia makala gazeti la Raia Mwema kwa muda mrefu. Ni mhitimu wa Shule ya Sekondari ya Mara na baadaye alienda kwa masomo ya kidato cha tano na sita huko Ilboru mkoani Arusha. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere Uganda mwaka 1993 kwa masomo ya Uandishi wa Habari na baadaye Uingereza kwa masomo ya Uzamili katika fani ya uandishi wa habari kwenye Chuo Kikuu cha Wales. Amewahi kuwa mhadhiri kwenye Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ) cha Jijini Dar-es-Salaam. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Mhadhiri kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam masomo ya Idara ya Uandishi wa Habari.

Mussa Mgwatu
Mussa Mgwatu

Dkt. Mussa I. Mgwatu ni Mhandisi na mhadhiri katika kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Pamoja na utafiti ndani nan je ya Tanzania Dkt. Mgwatu anatajwa kama miongoni mwa waandisi mahari nchini. Alipata shahada yake ya Uandisi toka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, na shahada yake ya Uzamili toka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada wakati shahada yake ya Uzamivu aliipata toka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.

(23)

About the author

bongoz

1 Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • Nyadhifa sasa wanapewa wasomi waliobobea kwnye fani husika, ryoba awe mbunifu anagalau tbc irudi kuwa kama ile ya tido mhando

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available