Habari Kuu NZITO ILIYOINGIA Uncategorized

CHADEMA Yaishukia Serikali; Yadaiwa Kuingilia Chaguzi za Mameya

Mwandishi Wetu (ZAMA MPYA)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeijia juu serikali kwa kile ambacho kinadai ni njama za kuhujumu demokrasia katika utaratibu wa kumpata Meya wa Jiji la Dar-es-Salaam. Katika taarifa yake iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Tumaini Makene kufuatia kikao cha awali cha Kamati Kuu ya Chama hicho jijini Dar jana, chama hicho kimedai kuwa kumekuwepo na njama nyingi ambazo zimejaribu kuvuruga chaguzi mbalimbali kwenye maeneo ambayo chama hicho na washirika wake katika UKAWA walikuwa waunde Halmashauri kufuatia kushinda viti vingi vya madiwani katika maeneo hayo.

“Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa CHADEMA haitakubali kuona Serikali ya awamu ya tano ikitawala kwa kutegemea udhalimu wa kutumia vyombo vya dola huku ikivunja sheria na taratibu nchi” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa Mbowe amedai kuwa “Ipo mikakati ya siri ambayo imeanza kutekelezwa kwa vitendo vya kuwakamata na kuwashushia hadhi na kuwadhalilisha wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge na madiwani ambao kama inavyoendelea kufanyika Jiji la Dar es Salaam.”

Ikitolea mifano madai hayo taarifa hiyo imesema kuwa katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na njama za wazi kabisa za kuvuruga upigaji kura wa kuwapata mameya wa miji mbalimbali n ahata kusababisha baadhi ya maeneo Chama cha Mapinduzi kushinda wakati kikiwa na idadi ndogo ya madiwani. “Huko Kyerwa ambako tulikuwa na madiwani wengi, madiwani wetu walikamatwa siku ya kupiga kura na kubambikiwa kesi, huko Kilombero hata leo tu mbunge wa jimbo amekamatwa na kudhalilishwa asiingie ukumbi wa kupiga kura” amedaiwa Mbowe kusema hivyo katika taarifa hiyo akiongeza kuwa “Tunapozungumza hapa Mbunge Mdee anashikiliwa na polisi, wanamshikilia Mbunge Waitara, wanamtafuta Kubenea, wanawashikilia madiwani wetu na wanachama bila sababu zote za msingi, lakini lengo ni kuhujumu uchaguzi wa meya”

Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza taratibu zozote za kisheria ambazo chama hicho kimechukua ili kuwawajibisha wahusika mbalimbali ambao wanadaiwa kutekeleza maagizo ya viongozi wa juu wa serikali au CCM. Hata hivyo taarifa hiyo imeionya serikali kuwa “Amesema kuwa hali hiyo ya sheria kuvunjwa kwa ajili ya kuwashughulikia wapinzani ikiendelea bila kukomeshwa ikiwemo kuwapora wananchi haki yao ya wazi kama inavyotaka kufanyika kwenye umeya wa Dar es Salaam, watawala watachochea moto ambao watashindwa kuuzima.”

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kinaendelea Jijini Dar leo na kinatarajiwa kutoa tamko rasmi la kuchukua misimamo mbalimbali kuhusiana na hali ya kisiasa nchini.

(4)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available