TANZANIA UCHUMI

Watalii Waongezeka Tanzania

Na. Mwandishi Wetu

Idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania imeongezeka kwa asilimia 10.4 katika kipindi cha miezi kumi ya mwaka jana (hadi Oktoba) jana kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka juzi. Ongezeko hilo limetokea licha ya hofu iliyokuwepo kwa baadhi ya wamiliki wa makampuni ya utalii na mahoteli ya watalii kufuatia kuongezwa kwa kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 kwenye huduma mbalimbali za utalii. Baada ya ongezeko hilo kulikuwa na hofu kuwa watalii watakwepa kutembelea Tanzania kwani baadhi ya huduma ambazo zilikuwa nafuu zitakuwa ghali kulinganisha na huduma kama hizo katika nchi jirani ambazo Tanzania inashindana nazo katika sekta ya utalii.

Idadi ya watalii mwaka jana ilivuka milioni moja na kulipatia taifa zaidi ya dola 2.2 bilioni; hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Wizara ya Fedha.

MAGHEMBEEWakati huo huo Waziri wa Utalii na Maliasili Profesa Jumanne Maghembe (pichani)amepongeza uamuzi wa China wa kupiga marufuku na hatimaye kuondoa uchakatuaji wa vitu vinavyotokana na meno ya tembo hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2017. Serikali ya China ilitangaza Disemba 30, 2016 kuwa imedhamiria kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo na vitu vinavyotakana na meno hayo ifikapo mwishoni mwa 2017.

“Napenda kuipongeza serikali ya China kwa uamuzi wake huo. Ni hatua mojawapo ya kuelekea kuwalinda tembo. Marufuku hii itasababisha kupungua kwa bei ya meno ya tembo na hivyo kufanya biashara hii kutokuvutia” amesema Prof. Maghembe.

“Hii biashara imekuwa ikivutia watu wengi kwani walikuwa wanalipwa vizuri sana ili waweze kupata nyara hizo, kitu ambacho kilikua kinachochea sana uwindaji na uuaji wa tembo” amesema Profesa Maghembe akizungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la China la XHINUA.

Ripoti ya serikali ya 2015 ilionesha kuwa kwa kipindi cha miaka mitano tu asilimia 60 ya tembo nchini walikuwa wameuawa. Hadi hivi sasa kuna kesi kadhaa zinazoendelea nchini zenye kuhusika na ujangili ikiwemo kesi ya mwanamama wa Kichina ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa biashara hiyo kwani tangu kukamatwa kwake mauaji ya tembo nchini yalipungua kwa kiasi kikubwa.

Wakati huo huo Profesa Maghembe amesema kuwa mbuga zote za taifa zitachora mipaka yake na kuweka alama za mipaka hiyo ifikapo mwishoni mwa Januari mwaka huu ili kuhakikisha kuwa mipaka hiyo inajulikana na kuondoa uvamizi au matumizi yasiyoruhusiwa katika mbuga hizo. Prof. Maghembe amesema hayo wakati akizindua bodi mpya ya TANAPA ambayo inaongozwa na Mkuu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gen. George Waitara ambaye aliteuliwa na Rais Magufuli hivi karibuni.

(48)

About the author

bongoz

2 Comments

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available