TANZANIA UCHUMI

BOT Yasimamisha Uendeshaji wa Benki ya Twiga BanCorp.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu.

Na Sabina Wandiba

Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesimamisha uendeshaji wa Benki ya Twiga BanCorp kwa muda wa wiki moja kutokana na kushindwa kujiendesha.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Gavana wa BoT Prof. Beno Ndullu amesema, uamuzi huo umechukuliwa baada benki hiyo kujiendesha kwa hasara ambapo ilianza na mtaji wa shilingi billion 7.5 ambapo hadi sasa inadaiwa na BoT shilingi billion 21.

Aidha , Gavana amewataka wateja wenye  Amana zao kutokuwa na wasiwasi na fedha zao lakini pia amewataka wenye madeni katika benki hiyo kulipa madeni yao na kwamba BoT itafuatilia.

Amesema, benki hiyo itasimama shughuli za kibenki wakati Benki Kuu ikiangalia namna uendeshaji wa Benki hiyo utakavyokuwa.

(15)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available