ELIMU UCHUMI

Bank Ya CRDB Tawi La Manyoni Yachangia Bweni La Wasichana Shule Ya Sekondari Mwanza.

Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

Benki ya CRDB tawi la Manyoni limetoa mifuko 73 ya saruji yenye thamani ya Sh. Mil 1, 168, 000 ili kuchangia ujenzi wa Bweni la Wasichana wa kidato cha tano na sita la Mwanzi Sekondari iliyopo Wilayani Manyoni,  Mkoani Singida.

Mchango huo uliwasilishwa na Meneja tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karata  ambae alisema mchango huo umetolewa na Watumishi wa Benki ya CRDB Tawi la Manyoni ambao wameguswa na tatizo la Wanafunzi wa Kidato cha tano na sita wa Mwanzi Sekondari wanaoishi katika mazingira magumu kwa kukosa bweni baada ya bweni walilokuwa wakilala kuungua kwa moto mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Msaada huo ulipokelewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe jana tarehe 03 Novemba 2016 ambaye amewashukuru sana wafanyakazi hao. ‘Nawaomba wananchi na wadau wengine wa maendeleo waendelee kutuunga mkono katika juhudi za ujenzi wa bweni hili la Wasichana wa Mwanzi Sekondari ili waepukane na adha wanayoipata sasa na kuongeza kusema Manyoni tumeamua wilaya iende mbele’ Alisema Mwambe.

Bweni la Wasichana wa Shule ya Sekondari Mwanzi Wilayani Manyoni liliteketea kwa moto usiku wa Tarehe 9 Septemba, 2016 na kuwaacha Wanafunzi hao wakiwa hawana mahali pa kulala.

(34)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available