Fredy Masolwa UCHUMI

Bahasha na Fursa 2017 – Sehemu ya 2

Sehemu ya kwanza “sasa tazama fursa, omba ushauri au mtaji kwa marafiki zako wa ukweli, then anza biashara yako kwa nidhamu”.

Mawazo ya marafiki wa kweli yanaweza anzisha biashara yako kwa mambo mbalimbali (wazo la biashara, eneo la kufanya biashara, sehemu ya kununua mali biashara, njia ya kujitangaza na kupata wateja, mtaji wa pesa na vitu, njia ya kutunza matumizi na mapato, na njia ya ulinzi wa biashasara yako na mtaji n.k)

– Kabla au baada ya kuanza biashara kwa 5 ya kwanza.

Chukua 5 ya pili, hii ni aina ya mawazo yako, vitu upendavyo, tabia zako na aina ya maisha yako kiujumla.

Mfano wa tabia zako 5 ambazo 2017, hautaweza kufanikiwa kamwe ni;-

  1. Unapenda kuchat makundi whatapps ya ngono na mapenzi muda wote 24/7
  2. Huna muda wa kusoma Magazeti, Vitabu mbalimbali vya maono na mafunzo n.k
  3. Huna muda wa kujifunza vitu mbalimbali muhimu, kutohudhuria semina, warsha na matamasha mbalimbali ya kukujenga wewe kifursa na kifikra.
  4. Hauna uwezo wa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi yako, na kufanya kuishi kwa matumizi yako kuwa makubwa zaidi kuliko mapato kwa mwezi, yanayo kusababishia kuishi na madeni wakati wote, ambayo ayatakuweka huru na kushindwa kufikria fursa, maisha n.k
  5. Hauna mfumo/utaratibu wa usafi wa moyo/mavazi yako/nyumba yako/maisha yako, pamoja na kutoweza kutunza kumbukumbu zako kimaandishi au kwenye mafile, na kupelekea kushindwa kuratibu maono yako kwenye action plan n.k

Mfano wa tabia zako 5 ambazo 2017, utaweza kufanikiwa kwa fursa yoyote ni;-

  1. Una magroup mengi ya whatapps ya uwekezaji, biashara, maono na fursa, yanayoweza kuwa chanzo kizuri cha kufunguka, but magroup mengine yape muda maalumu.
  2. Unapenda kusoma nyaraka, magazeti muhimu, vitabu vywa kiada na ziada vyenye mafunzo na mawazo mbalimbali ya kifursa, kusikiliza vipindi sahihi kwenye radio na vijiwe mbalimbali, kuangalia vipindi vizuri kwenye TV, YouTube n.k
  3. Uwezo wa kuhudhuria warsa, matamasha na semina mbalimbali na muhimu kwa kuongeza ufahamu wa mfumo wa biashara, fursa, maisha n.k
  4. Uwe na uwezo wa kutofautisha biashara na wewe (separate business legal entry), pamoja na uwezo wa kuratibu mapato na matumizi kutokana na bajeti zako n.k
  5. Uwe na utaratibu wa kuweka kumbukumbu zako kwenye maandishi na mafile mbalimbali, na kuziratibu kumbukumbu kwa muda sahihi n.k

Sasa hapa ukichukua 5 ya kwanza kwenye mazuri na 5 ya pili kwenye mazuri, utapata Uwekezaji Mzuri wa Biashara nzuri kwa kuanza kidogo kidogo mpaka unakuwa mkubwa.

5 + 5 = Uwekezaji/ Kutowekeza

2.2 SADAKA

Bahasha kuu ya pili, baada ya uwekezaji/ajira yeye faida n.k, unashauriwa kuweza kutoa sadaka kwa utaratibu wa 5 + 5 = SADAKA kutokana na mavuno ya uwekezaji/ajira n.k

…itaendele usikose kufatilia

 

Mwandishi – Fredy Masolwa, Simu – 0715 011 406

(59)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available