Fredy Masolwa UCHUMI

Bahasha na Fursa 2017 – Sehemu ya 1

1. UTANGULIZI

Biashara ya kifursa ni matokeo ya mzalishaji na mtumiaji, lakini mwenzeshaji wa yote ni mfanyabiashara katika ngazi tofauti kwa kujitolea, faida au hasara n.k

Mwaka 2017 anza na badiriko la kifedha, kwa kuwa na bahasha kuu nne kila mwisho wa mwezi ambazo ni

 1. Sadaka
 2. Akiba
 3. Uwekezaji/Kazi/Ajira
 4. Mambo Muhimu

Natambua watu wengi utumia zaidi ya kipato (Income < Expenses), wengine umaliza muda wao katika kazi aliyoajiriwa na kujikuta pato lake ubakia kuwa mshahara tu

Biashara haitaji pesa nyingi, ni wazo na matatizo ya watu ndio uleta fursa. Majibu ya swali langu la 5 + 5 = ?, ni mengi kwa kuangalia bahasha moja moja hapo juu.

2. BAHASHA KUU

Tuangalie bahasha kuu za 2017, kwa hatua sahihi, kupitia swali letu la 5 +5 =?

2.1 UWEKEZAJI /AJIRA / KAZI

Hii bahasha ni bahasha kuu ya mwanzo kabisa kuanza nayo, uwekezaji ni aina ya ubunifu wowote wa kibiashara au fursa yenye kuingiza kipato ikitokana na maono na ndoto zako.

Ajira au kazi pia ni aina ya uwekezaji kwa elimu na ujuzi wako mwisho wa siku uingiza kipato. Tukianza na bahasha ya uwekezaji tukiamini inajibu swali la 5 + 5 = Uwekezaji

– Kwanini jibu ni uwekezaji hapo

Chukua 5 ya kwanza, hii ni aina ya marafiki, jamaa au ndugu wa karibu utakao kuwa nao 2017, hao wanaweza kukufanya wewe ukawekeza 2017 au kutowekeza.

Mfano wa marafiki wako 5 ambao 2017, hautaweza kufanikiwa kamwe ni;-

 1. Mtu wa ubaya tu
 2. Anapenda habari za mapenzi
 3. Uelewa wa mambo hakuna
 4. Mlevi, mtu wa misifa na uchat muda wote
 5. Hana wivu wa maendele n.k

Mfano wa marafiki wako 5 ambao 2017, utaweza kufanikiwa kwa fursa yoyote ni:-

 1. Ana amini katika Mungu
 2. Usaidiana katika raha na shida
 3. Msomi/Mjuzi/Mtaalamu wa mambo mbalimbali
 4. Ana mipango inayoonekana na kutekelezeka
 5. Ana aminiwa na mtu, watu, taasisi na makundi mbalimbali.

Ajira na Kazi pia inasaidia kuipa nguvu biashara utajayoianza kwa kusaidia initial operations cost, kwa ambaye hana kazi/ajira kwa kupitia marafiki wa kweli unaweza kuwekeza kwa nguvu zao.

Sasa tazama fursa, omba ushauri au mtaji kwa marafiki zako wa ukweli, then anza biashara yako kwa nidhamu…..

Itaendele kwa kuangalia 5 ya pili.

 

Mwandishi – Fredy Masolwa, Simu – 0715 011 406

 

(107)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available