Afya & Mazingira TANZANIA

UTAFITI: Ulaji wa Nyama za Viwandani na Mgonjwa wa Pumu

Na Laila Sued.

Ulaji wa nyama zilizopitia viwandani unaweza kusababisha mtu mwenye pumu kuzidiwa zaidi ,umebaini utafiti. Kula zaidi ya vipande vinne vya nyama hizo kwa zaidi ya mara nne kwa wiki ni hatari, ulibaini uchunguzi huo uliofanywa miongoni mwa watu 1,000 nchini Ufaransa, na kuchapishwa kwenye jarida la Thorax.

Watafiti wanaamini kuwa hueda sababu ya matatizo hayo ikawa ni matumizi ya kemikali ya nitrite inayowekwa kwenye nyama hizo kuzizuwia kuoza ambayo hutumiwa kwenye vyakula kama Soseji , na samaki (salami).

Lakini wataalam wanasema kuwa uhusiano wa hatari hizo haujaidhinishwa na uchunguzi zaidi unahitajika kufanyika kuthibitisha hilo.

Badala ya kuwa na hofu juu ya ulaji wa aina moja ya chakula , watu wanapaswa kula chakula chenye virutubisho vya kiafya na vya aina mbali mbali, walishauri wataalam Tayari vyakula vinavyopitia viwandani vimehusisha na maradhi ya saratani.

Wataalam wanasema watu wanapaswa kula nyama nyekundu ambacho si zaidi ya gramu 70 kwa siku, ama kiwango hicho hicho cha yama zilizopitia viwandani kwa ajili ya kuwa na afya bora. Kiwango hiki ni sawa na takriban Soseji moja ama viande viwili vya nyama kwa siku.

Utafiti huo uliofanyika nchini Ufaransa kama sehemu ya uchunguzu wa taifa hilo juu ya chakula na afya katika kipindi cha muongo mmoja kuanzia 2003 hadi 2013. Takriban nusu ya watu ya waliofanyiwa walikuwa ni wagonjwa wa pumu.

Utafiti huo uliangalia hasa juu ya dalili za pumu – kukosa pumzi, matatizo ya kupumua na wenye shida mbali mbali za kubanwa vifua – na kiwango cha nyama wanachopaswa kula : mlo mmoja ulikuwa ni vipande viwili vidogo (slaces) vya nyama ya nguruwe , soseji moja na vipande viwili vidogo vya samaki (salami).

Miongoni mwa watu wenye pumu , ulaji wa kiwango kikubwa cha nyama ulihusiana na kuwa na dalili mbaya zaidi za matatizo ya mapafu.

Daktari Erika Kennington, mkuu wa utafiti wa maradhi ya pumu katika kituo cha pumu nchini Uingereza anasema: “licha ya kwamba vyakula fulani vinaweza kusababisha pumu miongoni mwa watu, kwa jumla hakuna chakula maalum cha kudhibiti dalili za pumu.

Kwa watu wengi wenye pumu , ushauri wa ulaji wa vyakula vyenye afya ni sawa na ule unaotolewa kwa mtu mwingine yoyote yule: la muhimu ni kula chakula chenye virutubisho vya mwili vinavyohitajika ambavyo vinajumuisha chakula ambacho hakijakaa muda mrefu na chakula ambacho hakijapitia viwandani na vyenye sukari kidogo, sukari na utumiaji wa mafuta ya maji maji.”

(46)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available