TANZANIA

Neno la Matumaini: Uwezekano wa Barrick Kusema “Hatuna Deni” ni Sifuri

Profesa Kabudi Waziri wa Sheria na Katiba akiwa na ugeni kutoka Barrick kwa ajili ya majadiliano ya makinikia.

NI wazi kuwa kwa kuangalia hali ilivyo; it was to the interest of Barrick to negotiate than litigate; at least for now. Imagine kama wakikubali deni hata theluthi moja ya madai yetu; watu watamcheka Magufuli? Wameambiwa wanadaiwa karibu dola bilioni 190; wakisema wamekubali hata dola bilioni 60 ni ndogo hizo? Na wakakubali kuzilipa in cash and shares au namna nyingine kwa kampuni ya serikali (say STAMICO) si utakuwa mwanzo mwingine na utatengeneza mwelekeo mpya?

Kosa wanalofanya CHADEMA (katika mabezo ya Mwenyekiti Mbowe jana) ni kuwa too literal kwenye hili; ni kutokuelewa jinsi ya kuwa mtu wa mikakati. Leo hii tunaweza kusimama na kampuni hii kubwa hivi ambayo ni tishio sana duniani kwenhe madini na ina historia nyingi yenye utata; kunatupa heshima siyo aibu. Sioni ni kwa namna gani Barrick wataishia na kusema “hatuna deni lolote”.

Wapo waliosema kuwa ati tukigangamala tutanyolewa bila maji; wengine walisema au tutashtakiwa, wengine wamefikia mahali pa kusema ati hawa watu ni makomandoo! Yaani, wamekuwa kama wale watu waliotumwa na Nabii Musa kwenda kuchunguza ile nchi ya Kanaani. Waliporudi wengine walikuja na habari mbaya za jinsi gani watu wa kule walivyokuwa wanatisha na ni jinsi gani Bani Israeli walikuwa hawana nafasi! Ilikuwa ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune waliorudi na kusema “inawezekana”.

Sasa leo tuna watu wengi ambao wanataka taifa la watu huru liishi kwa woga. Hoja ya kiasi gani kinadaiwa ni negotiation tactic. Mtu yeyote ambaye amewahi kukaa kwenye negotiations anajua hili hata mtu wa kawaida tu. Mtu unaenda kununua kitu na unakuta bei ni 150,000 na unamzungumzisha mtu hadi anakuuzia kwa 100,000 wewe unaweza kufurahi lakini yeye anaweza kufurahi zaidi kwani alipigia hesabu kitu chenyewe angekiuza kwa kiasi chochote juu ya 60,000 atakuwa na faida sasa utamcheka kama amepata faida ya 40,000?

Barrick sioni ni kwa namna gani watakapopambanishwa na ushahidi wataamka na mabegi yao na kusema “hatuna deni”. Kubwa wanaloweza kufanya ni kusema “deni ni kubwa hatuwezi kulilipa tuangalie namna gani tunaweza kulipunguza liwe manageable or payable”. Kutoka hapo ni sisi tuna dictates terms of repayment. Ni sisi tutaamua tuwakubalie kama in good faith walipe kiasi gani. Na wakikubali hata kusema robo ya tulichosema tunawadai, Magufuli ataonekana ni mwana mkakati mzuri sana kuweza kutokea Afrika.

Lakini pia tukumbuke kuwa wao Barrick nao wana kitu wanakitaka kwetu; wanataka access ya raslimali zetu na madini kwani itawasaidia kuongeza “bottom line” yao yaani “faida” na wanahisa wao watafurahia. Hivyo, watakuwa tayari kufikia kiwango fulani ambacho watajua wataweza kukimudu na wakati huo huo kuonekana wamefanya jambo zuri kibiashara. Wamekuja siyo kutufurahisha sisi bali kufurahisha wanahisa wao.

Kitu pekee ambacho binafsi ningependa kukiona siyo kama kile cha mambo ya hela ya Rada ambapo tulipoteza na wengine tulikataa fedha zisilipwe serikali. Magufuli atakuja na wazo zuri zaidi la jinsi gani malipo hayo yatafanyika (treni, treni, treni, Stieler’s Gorge???). Kumbuka, Bwala la Stielger’s litagharimu kama dola bilioni 3 au nne tu! na reli yetu hiyo mpya ni kiasi kidogo tu…

Well.. ujanja siyo kuwahi au kufika; ni kupata…
MM Mwanakijiji

(481)

About the author

bongoz

2 Comments

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • Tangu uluposema tufunge kwa ajili ya uchaguzi 2015 nimependezwa sana na makala zako. Nimeacha kuwa kwenye kundi moja na wale 10 wanaojitegemea. Bwana ndiye mshindi wetu!

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available