Afya & Mazingira Fredy Masolwa TANZANIA

Makamu wa Rais Samia Hassan Aanza Ziara Mkoani Mwanza, Atumia BOMBARDIER Q400

Na Fredy Masolwa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza na kwa usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza pamoja na abiria wengine.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

Makamo wa Rais amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.

MWANZA

Alipowasili Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini.

Ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.

Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais amesema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.

Makamu wa Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu abiria waliosafiri nae kwenye ndege mpya ya Bombadier Q400 ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) akitokea Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu abiria waliosafiri naye kwenye ndege mpya ya Bombadier Q400 ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) akitokea Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi

Katika kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya Afya imepokea kiasi cha shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.

Pia amesema saratani ya mlango wa kizazi inasababisha vifo vingi vywa kinamama hali ambayo hutokana na magonjwa yanagundulika na wakati ugonjwa tayari umefikia hatua isiyotibika, na husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama kutokea.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300 vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani. Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wababa kote nchi kuunga

Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku nne mkoani humo katika wilaya za Sengerema, Ukerewe, Ilemela, Nyamagana, Misungwi, Kwimba na Magu.

 

(22)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available