TANZANIA

Majibu Juu ya Kutoweka JF: Eti “Mwanakijiji Ukome”

"Hatuombi radhi kwa uhuru wa maoni"

Na. M. M. Mwanakijiji

Majibu: Kuna watu wengine = labda kwa kutokujua – wanadhania kuwa tatizo la kudhibiti mitandao limekuja baada ya Magufuli. Na hivyo kwa makosa kabisa wananilaumu mimi na wengine ambao tulikataa mabadiliko ya kuzungusha mikono kwa hili. Wanafanya makosa kadhaa makubwa.
 
1. Wanataka tuamini kuwa tatizo la kudhibiti mitandao limetokana na Magufuli. Hivyo, wanasahau kabisa kuwa sheria ya Uhalifu wa Kimatandao ililetwa wakati wa Kikwete na kutiwa saini na Kikwete, wakati mgombea yule akiwa bado CCM na hakuwahi kuonesha kuilalamikia. Ni sawasawa kabisa na watu wa CCM kulalamikia sheria hii au lililotokea. Ni kujipa usahaulifu wa kujichagulia.
 
2. Wanasahau kuwa suala la kudhibiti mitandao siyo suala la Tanzania peke yake, Ethiopia hadi Marekani, Uganda hadi Ufilipino mataifa na serikali mbalimbali yanajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii katika kuhakikisha kuwa inatumika vizuri.
 
3. Suala la mgongano wa mawazo na fikra na serikali kudhibiti uhuru wa maoni katika Tanzania halikuanza na Kikwete wala Magufuli; na wala halikuanza wakati wa Nyerere. Hili ni suala tulilorithi toka wakati wa Ukoloni na ni tatizo ambalo lina lengo la kutaka serikali iliyoko madarakani itawale bila kusumbuliwa. Inasikitisha watu wamejipa usahaulifu na kusahau kabisa jinsi gani uhuru wa habari na maoni ulikuwa unapata shida wakati wa Kikwete; watu hawa wamesahau kabisa kuwa kina Max (watu wa JF) walitiwa ndani mara ya kwanza kuhusiana na JF wakati wa Kikwete.
 
4. Ndugu zetu hawa – labda ni vijana waliingia siasa mwaka 2015 – wamesahau au hawajui kabisa kuwa uhuru wa maoni na mawazo inahusisha pia uhuru wa wale tusiowapenda nao kutoa mawazo yao huru. Mimi nilimkataa Lowassa na mambo yake yote alipokuwa CCM na nilimkataa akiwa CHADEMA kwani naamini ujio wake CHADEMA ulivuruga kwa kiasi kikubwa harakati za upinzani ambao baadhi yetu tulitumia muda mrefu sana kuzijenga. Kwa hilo sina sababu ya kujuta au kujifafanua, rekodi yangu iko wazi. Inashangaza kama kuna watu ambao wanamini kuwa kama Lowassa angekuwa Raisi basi uhuru wa mitandao na maoni ungezingatiwa sana; rekodi ya hiyo kwa Lowassa iko wapi? Katika hilo Lowassa hana tofauti na Magufuli na tuliomuunga mkono Magufuli tulimuunga mkono bila kudhania kuwa atakuwa ni kama kiongozi wa upinzani kweli kweli.
 
Kutokana na hayo yote, niwasaidie tu wale ambao kwa namna fulani wanafikiri wameniambia “ukome” kuwa bado naamini na nitaendelea kupigania uhuru wa habari na maoni kwa namna yangu na ndio maana nilishawahi kusema mapema zaidi tangu sheria ya “mitandao ya jamii” ipitishwe kuwa mimi nimmoja wa watu ambao siko tayari kuitii sheria hiyo kwa sababu naamini katika dhamira yangu ni sheria ambao ni kinyume na maadili, ni ya hatari na hata kama imepitishwa na vyombo halali bado si SHERIA halali.
 
Kutokana na hili ndio maana niko tayari kushirikiana na wenzangu ambao tumekuwa kwenye harakati hizi kwa zaidi ya miaka ishirini kuona chombo kingine huru zaidi na kisichoingiliwa na serikali kwenye mitandao kinakuwepo na kinaendelea kusimamia uhuru wetu wa maoni, kukusanyika na kujadiliana bila kuangaliia mabegani nani anatuchungulia. Hili nililiamini mwaka 1997 wakati naanza harakati hizi; na ninaliamini mwaka huu kuwa bado ni sahihi.
 
Hivyo, tulizeni ball.
 
MMM

(300)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available