Maoni TANZANIA

Macho Manne: Lipumba Huyu Ndiyo Alisifiwa Sana na WanaCUF

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa muda mrefu Profesa Ibrahim Lipumba alisifiwa sana na kuinuliwa miongoni mwa wanasiasa wa upinzani. Alisifiwa kiasi kwamba ilikuwa ni kama nyota ya jaha aliposimama mbele ya wana CUF. Alikuwa ni alama ya CUF, alikuwani “msomi aliyebobea” na alisifiwa kwa mafanikio yake mbalimbali ya kitaaluma ndani na nje ya nchi.

Tuliambiwa kuwa kutokana na ujuzi wake uliobobea katika uchumi Tanzania ilimhitaji sana; ilimhitaji kwa kuwa alikuwa ni mbobezi katika ushauri wa mambo mbalimbali ya uchumi. Ni kwa sababu hiyo CUF walimsimamisha mara nne kugombea Urais! Hawakuwa na mwingine na haikuonekana uwezekano wa kuwa na mwingine. Lipumba hakuwa pumba!

Alionekana kuwa ni mwanasiasa mahiri kwa jinsi ambavyo alishiriki kuwavutia wasomi wengi kwenye chama cha CUF na wakati huo huo alionekana kubeba matumaini ya kundi moja nchini ambalo lilimuona kama alama ya uwezo na kufanikiwa kwa mwana kundi hilo (rejea video yake “ile”).

CUF ilikuwa inahusishwa na Lipumba huku Bara na Seif Hamad kule Zanzibar na hawa wawili kwa kweli ndio walikuwa CUF hasa. Leo hii kugawanyika kwa hawa wawili tu tayari kumeigawa CUF katika vipande ambavyo hatujaona mwisho wake bado. Mgawanyiko uliotokea si wa kidini bali ni wa kisiasa na tena ni siasa ambazo ni ngumu mno kuzielezea kwani siyo suala la kiitikadi au kimsimamo bali zaidi ni maslahi ya aina fulani.

Lipumba huyu huyu ambaye alisifiwa sana na alitaka hata kugombea Urais – mara nne! Anatuonesha uwezo wake (au kukosa uwezo kwake) kutatuta tatizo la kisiasa ndani ya chama chake na badala yake kama wanasiasa wengine wa zama zetu naye ameamua kuwa gangwe tu.

Zile sifa zile… zimejaribiwa… na watu wanaweza kuamua kama kweli zilimfaa kweli au la. Au ndio kusoma kwingi..

(216)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available