TANZANIA

Live: Mange Aongoza Maandamano Yake Washington DC

Waandishi Wetu – Washington DC na Mikoani

Mwanamama Mange Kimambe asubuhi ya siku ya Jumatano ameongoza kundi la Watanzania kuandamana nje ya Ubalozi wa Tanzania katika Jiji la Washington DC, nchini Marekani. Pamoja na kuongoza maandamano hayo pia amepata nafasi ya kuhojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Marekani (VOA).

Alhamisi ni Siku Kuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Siku hiyo pia imepangwa kuwa ya maandamano yaliyoitishwa na mwanadada Mange Kimambi. Makundi mbalimbali ya vijana yamekuwa yakijitangaza kushiriki maandamano hayo yenye lengo la kumshinikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kujiuzulu. Maandamano hayo haya hivyo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi na kuwa hadi hivi sasa hakuna chama cha kisiasa ambacho kimeejitokeza kuyaunga mkono. Hata hivyo, mhamasishaji mkuu wa maandamano hayo Mange Kimambi amedai kuwa maandamano hayo si ya kisiasa na hayana lengo la kuiondoa CCM madarakani na hayahusiani na chama chochote.

Hadi hivi sasa inaonekana Serikali inachukulia kwa uzito mkubwa tishio la maandamano hayo hasa kufuatia baadhi ya balozi za nchi za Magharibi kuonya raia wao kuhusiana na siku hiyo. Marekani na Uingereza zote zimetoa taarifa kuwaasa raia wake walioko Tanzania na wale wanaopanga kutembelea Tanzania kuwa waangalifu hasa siku hiyo hasa kwa vile serikali imetishia kuyazima maandamano hayo na uwezekano wa kutumika risasi za moto kuwepo.

Tutawaletea hadi hivi sasa yale yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini kuelezea kile ambacho kinatarajiwa kufanya na jinsi serikali inajitahidi kudhibiti. Unaweza kutuma taarifa mbalimbali – picha na video – moja kwa moja kupitia anuani ya klhnews@gmail.com.

(301)

Paul Mpazi April 25, 20183:41 am

Wakati huo huo ubalozi wa Marekani nchini umetoa tahadhari kwa wananchi wao wanaoishi Tanzania kuhusu maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Ubalozi umetoa tahadhari kwa raia wake wote kwamba siku ya Aprili 26 wanatakiwa kuwa makini kwa sababu inawezekana kabisa maandamano yakatokea.

bongoz April 24, 20183:53 pm

Mange akiwa njiani kuelekea Washington DC amedai kuwa amekutana na maajenti wa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) waliomtaka asiendelee na safari yake kwani kuna tishio la maisha yake. Mange aliwaambia hawezi kuacha kwenda DC hata kama anafanya hivyo akitetemeka..

bongoz April 24, 201812:35 pm

Vikosi vya Polisi pia vimepita mkoani Mbeya kuanzia maeneo ya nane nane, Kwa Mama John, katika kuonesha utayari wao kukabiliana na jambo lolote

bongoz April 24, 201811:47 am

Mange Kimambi amewaaga wanachama wake wa kudumu kupitia mtandao wa Instagram kuwa anaelekea Washington DC ambako anatarajia kuongoza maandamano ya Watanzania nje ya Ubalozi wa Tanzania jijini humo

About the author

bongoz

1 Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available