Afya & Mazingira TANZANIA

Kina Mama Watakiwa Waende na Maji Hospitali Teule ya Chemba, Dodoma

Ummy Mwalimu
  • Hakuna Maji
  • Gari la wagonjwa limeharibika mwaka sasa
  • Chumba cha mochwari kilijengwa vibaya
  • Watoto wanalazwa na watu wazima

Na. Dotto Kwilassa

Na Dotto Kwilasa

KINA MAMA WAJAWAZITO pamoja na wagonjwa  katika kituo cha Afya Hamai kilichopo wilayani  ya  Chemba mkoani Dodoma wanalazimika kwenda na maji kwa ajili ya matumizi yao kutokana  na kukosekana kwa huduma ya maji katika kituo hicho.

Hayo yalielezwa juzi na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk.Fatina Maingu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili hospitalini hapo.

Maingu alisema kuwa kwa muda mrefu sasa hawana huduma ya maji hivyo inawalazimu wagonjwa wote wanaoenda kutibiwa katika kituo hicho kwenda na maji yao kwa muda wote wanapokwenda kutibiwa hasa pale inapotokea kuwa wanaandikiwa kulazwa.

“Suala la maji katika kituo chetu cha afya ambacho hivi sasa kimechaguliwa kuwa Hospitali teule ya wilaya kinakabilia na changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa”alisema Maingu.

Aidha alibainisha kuwa kituo hicho cha afya ambacho hivi sasa kinahudumia wagonjwa 70 mpaka 100 kwa siku ikiwemo wagonjwa kutoka vijiji vya jirani kimekuwa katika hali hatarishi kwa wauguzi na wagonjwa wenyewe.  “Hakuna kabisa maji katika kituo chetu cha afya pamoja na wilaya kukichagua kuwa hospitali teule ya wilaya lakini bado maji ni kikwazo sana kwetu pamoja na wagonjwa kwani tunakosa hata maji kwa jili ya kuchemshia baadhi ya vifaa tiba”alisema Maingu.

Hata hivyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili ni kutokuwa na gari  lakubebea wagonjwa pamoja na uhaba wa watumishi katika kituo hicho kwani wapo 17 tu wakati walitakiwa wawepo watumishi 68.

“Tulikuwa na gari lakubebea wagonjwa lakini lina mwaka sasa halifanyi kazi kutokana nakuharibika hivyo limepaki wilayani na pia idadi hii ya watumishi haijitoshelezi kabisa kuwahudumia wagonjwa 70 hadi 100 kwa siku”alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na changamoto hizo pia kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa wodi ya watoto hali ambayo  imewalazimu kuwachanganya na watuwazima jambo ambalo sio salama kiafya.

“Majengo yaliyopo hayatoshelezi mahitaji hivyo watoto wanaotakiwa kulazwa tunawachanganya pamoja na watu wazima hali ambayo si nzuri kiafya”alisema Maingu.

Pia alisema kuwa pia kituo hicho hakina huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti hali ambayo inawalazimu kuwapa ndugu wa marehemu ili kuweza kutafuta pa kuwahifadhi.  “Kuna chumba kilijengwa lakini hadi hii leo hakina majokofu kwa jili kuhifadhi maiti lakini pia namna ambavyo kilijengwa hakikidhi kabisa mahitaji na sijui kwanini wakati wanajenga hawakutushirikisha sisi wahusika hali ambayo imesababisha jengo kubaki bila kazi yoyote”alisema Maingu.

Juhudi za kupata maafisa wa Wizara ya afya kuelezea kinachoendelea katika wilaya hiyo hazikufanikiwa. Pichani juu ni Waziri wa Afya Bi. Ummy Mwalim.

Mwisho.

(134)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available