Maoni TANZANIA

JPM Amteua Kashililah, Mangu, Malima na Makatibu na Manaibu

  • IGP Ernest Mangu Ateuliwa Balozi
  • Thomas Kashililah Naibu Katibu Mkuu Kilimo
  • Mnyeti RC Manyara, Adam Malima RC Mara

Na. M. M. Mwanakijiji

Rais John Magufuli leo amefanya mabadiliko katika watendaji wakuu wa serikali ngazi za makatibu wakuu na manaibu wao katika wizara mbalimbali pamoja na kufanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa. Mabadiliko hayo yametangazwa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Kwa mujibu wa Kijazi Aliyekuwa Katibu wa Bunge aliyebadilishwa hivi majuzi Dkt. Thomas Kashililah amepelekwa Wizara ya Kilimo ambako anaenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Viongozi wengine ambao wameteuliwa ni pamoja na aliyekuw Mkuu wa

Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Ernest Mangu ambaye ameteuliwa kuwa balozi pamoja na Aziz Mlima ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje ambaye naye ameteuliwa kuwa balozi. Vituo vya mabalozi hawa wapya vitatangazwa baadaye.

Adam Kighoma Ali Malima ambaye aliwahi kuwa Mbunge na kuwa ndani ya baraza la mawaziri ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Alex Mnyeti ambaye amejikuta kwenye tuhuma za kuwanunua madiwani wa CHADEMA amepandishwa cheo na kupelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Makatibu na manaibu wengine wameendelea kushika nafasi zao huku wengine wapya wakiingia na wengine kuondolewa bila ahadi ya kupangiwa nafasi nyingine.

Orodha kamili ya mabadiliko itawekwa hapa baadaye.

(53)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available