TANZANIA

Habari Nzito: Tundu Lissu Ajeruhiwa kwa Risasi, Dodoma

Na. M. M. Mwanakijiji

Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu amejeruhiwa kwa risasi akiwa ndani ya gari lake baada ya watu wasiojulikana kulishambulia gari hilo kwa kile kinachokadiriwa kuwa ni risasi zaidi  ya ishirini. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw. Freeman Mbowe Lissu alipigwa risasi akiwa anarejea nyumbani kwa chakula cha mchana kutoka Bungeni ambapo vikao vya Bunge vimeanza. Shambulio hilo linadaiwa kutokea nyumbani kwake maeneo ya Area D mjini Dodoma na juhudi za kuokoa maisha yake zimeendelea katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Hadi hivi sasa haijajulikana ni watu gani wamefanya jaribio hilo na bila ya shaka kutokana na harakati zake mbalimbali za kisiasa na kisheria linaweza kuhusishwa na mengi. Vyombo vya usalama hadi hivi sasa wakati tunakuja hewani havijatoa taarifa yoyote ile. Wiki chache zilizopita hata hivyo Tundu Lissu alidai kuwa kuna gari ambalo limekuwa likimfuata mfuata na kuwaonya wakuu wa vyombo vya usalama – akiamini kuwa gari hilo ni la usalama – waache kufanya hivyo. Vyombo vya usalama wakati ule havikutoa kauli yoyote kupinga au kukanusha jambo hilo.

 

 

(123)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available