Afya & Mazingira Fredy Masolwa Maoni TANZANIA

Dawa ya “ARTEQUICK” Ilivyotishia Uhai Wangu!!

Na. Fredy Masolwa

Naweza kusema uhai wangu ulikuwa matatani kupitia dawa hii ya Malaria “Artequick” inayotengenezwa nchini China wiki hii, ni kama sielewi kilichotokea mpaka sasa.

Wikendi hii niliamka huku hali yangu ya kiafya ikiwa na changamoto za maumivu kwenye kichwa, ilinipasa kwenda Hospitali kujua afya yangu, nilifika salama nikapokelewa Mapokezi na kuweza kuonana na Daktari wa zamu (Dkt), tulifanya majadiliano mbalimbali juu ya afya yangu na Dkt, baadaye nilipimwa damu, choo na haja ndogo kwenye chumba cha vipimo.

index2Baada ya muda mchahe nilipokea majibu toka maabara na kuniladhimu kuyarudisha kwa Daktari, nikiwa hapo nilielezwa nina Malaria 2, nakuomba kupewa dawa ya kutibu tatizo. Mara nyingi ninapoumwa huwa natumia zaidi dawa ya Malafine ya Tanzania na uniponya kabisa lakini daktari huyu akaniambia kuwa sio dawa nzuri ya Malaria kwasasa, kwani zinatibu wamama wajawazito kama kinga ya Malaria kwao. Hivyo akaniambia kuwa atanipa dawa nzuri sana ya Malaria ambayo ni “ArteQuick_tz” na kuipa sifa kemkem. Niliichukua na kunywa hapohapo dozi ya vidoge sita, unameza viwili kila baada ya masaa 24 pamoja na dawa ya kutuliza maumivu.

Baada ya kunywa kama saa moja, nilianza kuona macho mazito, mwili unakosa nguvu, kichwa kikigonga pande zote na kizungu zungu chenye kipanda uso kwa kasi kubwa, kushindwa kuona mbele na mambo kadha wa kadha, nikaanza kuogopa sana na kudhani ndio mwisho wa maisha yangu.

Muda unavyozidi hali yangu ilikuwa ikibadilika badala ya kuimarika, niliwatisha watu nilikuwanao karibu, nilishindwa kula, kila aina ya dawa ya kutuliza maumivu “anti-pain” zilikwama, nilimuita bwana kwa maombi makubwa lakini bado.

Ilivyofika usiku usingizi ulikata kuja maumivu yalizi kila wakati, ndani hapakaliki, simu siwezi kujibu wala kupokea, ni hali ya ajabu sana.

Siku ya pili yake hali ilikuwa vilevile, nikajiuliza maswali mengi sana “Hivi TFDA au TBS wanaitambua dawa hii ?” kwa serikari hii  “Wizara ya Afya wanaijua hii dawa?” nikaendela kulia tu “nikaomba kutazamiwa kasha la dawa hii kama lina nembo yoyote ya serikari au Taasisi ya JMT” NIKAMBIWA HAKUNA, nikambiwa imetengenezwa China…nikaendelea kuumia na kulia tu.

Nikakumbuka nchii ina ofisi ya MPANGO WA KUZIA MALARIA NCHINI (NMCP), sijui kama wanatambua hii dawa au wameacha tu, nikaendela kuuliza madaktari baadhi kwa njia ya simu nilipopata nafuu wengi wao walieleza hizi dawa zinawasumbua sana watu lakini ni nzuri.

Malaria inauma sana nchi, kuna dawa nyingi sana za malaria nchi na waratibu wa madawa hawaelezi wananchi ipi ni sahihi, sijui TBS, TFDA au Wizara ni yupi anatazama ubora, uhakika wa kutibu au uhalali wa dawa ni sawa na “sample” ilitumika kuipa uhalali.images

Dawa hii gharama zake ni kubwa kiasi, madaktari wengi hawaelezi vizuri wagonjwa juu ya dawa husika, hawajui ni mtu gani hataki kutumia wengi wao, au ni mtu wa aina gani hapaswi kunywa dawa hii kwani kwenye maelekezo yake hakuna.

Daktari mmoja aliniambi ninywe maji sana na matunda ilikupata choo hali itabadilika, niliweka mrija wa maji mdomoni kwangu, lakini hali ilikata kabisa, sina shida ya kisukari wala BP labda ingekuwa sababu.

Nashauri Wizara, TFDA na Mamlaka mbalimbali nchi kutoa maelezo mazuri ya dawa sahihi ya Malaria kwa aina ya watu ilikuepusha Vifo na Maumivu mbalimbali kwa wananchi kwanini mpaka sasa hakuna dawa sahihi ya Malaria, kuna aina tano na zaidi za dawa za Malaraia nchini.

Nilijaribu kufanya utafiti wa waliowai kuitumia, asilimia kubwa waliumia kwanza na kupona, wengine walipata tabu kama mimi na wengini walisifia kuwa ni dawa sahihi ya kutibu Malaria kwa sasa.

Siku ya pili niliandika Mirathi kabisa kwani nilijua naondoka, lakini sasa nimerudi katika hali yangu huku masikio yakiwa hayasiki vizuri

MUNGU NI MWEMA.

Niandikie – masolwa60@gmail.com

(319)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available