Fredy Masolwa MICHEZO TANZANIA

YANGA Bingwa Ligi Kuu Tanzania Bara “VPL” 2016/2017, Toto African na Wenzake Chaliii!!!

Na Fredy Masolwa

MWANZA – Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara “VPL 2016/2017” imemalizika leo kwenye viwanja vinane, huku klabu za Simba ikimaliza uwanja wa Taifa, Dar es  Salaam na Yanga ikimaliza uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, nakufanya wote kumaliza kwa kuweka kibindoni kila mmoja pointi 68 kwa michezo 30.

Katika uwanja wa Taifa Simba kaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC, huku Yanga wakichapwa 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba.

Baada ya mechi zote kumalizika kwenye viwanja vinane, Yanga inafanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa wastani wake mzuri wa mabao, ingawa bado kuna sintofahamu ya klabu ya Simba kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) mjini Zurich, Uswisi kudai pointi tatu zao walizopokonywa baada ya kupewa kimakosa kufuatia kufungwa na Kagera Sugar.

Kwenye uwanja wa CCM Kirumba bao pekee la Mbao FC limefungwa na Habib Hajji dakika ya 23, huku Yanga wakiangaika kurudisha bila mafanikio mpaka dakika 90 na 5 za nyogeza.

MECHI ZA VIWANJA VINGINE

Viwanja vingine Kagera Sugar imeifunga Azam 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, huku Stand United imeilaza 2-1 Ruvu Shooting Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, lakini Prisons imelazimishwa sare ya 0-0 na African Lyon Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati Ndanda FC imeshinda 2-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Mtibwa Sugar imeshinda 3-1 dhidi ya Toto Africans Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji imeshinda 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja Maji Maji Songea.

TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA LA KWANZA TOKA LIGI KUU

Baada ya matokeo yote kwenye viwanja vinane, timu tatu zinarejea kwenye ligi daraja la kwanza toka VPL, Ambazo ni JKT Ruvu kutoka Pwani, Toto African ya Mwanza na African Lyon ya Dar es Salaam.

Timu hizo zimeteremka baada ya mechi za mwisho za ligi huku mbili kila moja ikipoteza na moja ikipata sare ya bila mabao.

Mwisho!

(223)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available