MICHEZO

Jerry Muro Aomba Kufutiwa Adhabu Yake na TFF.

Na. Fredy Masolwa

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga aliyesimamishwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kutojihusisha na mambo ya soka kwa mwaka mmoja, Ndugu Jerry Murro. Ikiwa ni takribani miezi sita mpaka sasa akitumikia adhabu yake ameomba msamaha TFF apunguziwe adhabu na kusamehewa

Akiandika ombi lake la kusamehewa kwa njia ya barua kwenda TFF, Muro amesema kwamba anakiri kupata barua ya kufungiwa kutoka Kamati ya Maadili, lakini anaomba msamaha baada ya kutumikia nusu ya adhabu yake.

09a04d07-bd85-4a6a-af9a-7e873a83fa6f

Muro ameomba apunguziwe adhabu na kurudi kutekeleza majukumu yake kwa mwajirin wake, Yanga SC kuanzia kipindi hiki cha michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea visiwani Zanzibar.

Muro alifungiwa tarehe 08/07/2016 na kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Wilson Ogunde. kwa makosa mawili yakudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini alikaidi kulipa hadi leo. na kosa la pili ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC.

(59)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available