Fredy Masolwa MICHEZO

Fikra Huru:- YANGA SC SASA INAHITAJI MFUMO MPYA!!

Na. Fredy Masolwa

Ugumu wa watu kutokuwa bora katika mambo mbalimbali na muhimu Tanzania ndani ya majukumu yao kwenye kazi, biashara au taasisi na idara za kiofisi, miradi na mambo kadha wa kadha, kama mtu (Individual Entities) badala ya Taasisi au mfumo (Separate Legal Entities or Cooperation Entities), hili ni kosa linatokana na watu wengi kupatiwa elimu mashuleni na vyuoni, lakini taaluma na ujuzi wanachokifanya kwenye maeneo yao hawana nani bure kabisa, pamoja na kuishi maisha ya kuona mimi bora kuliko huyo au mfuno ndio tatizo la sehemu nyingi Tanzania.

LWANDAMILA

Huyu ni kocha mkuu wa klabu ya Yanga Sporting Club ya Jijini Dar es Salaam, akitambulika kwa majina yake kama “George Lwandamina”, akiwa na miaka 53 kwa sasa.

Tukirudi kwenye historia yake kidogo, alikuwa akifundisha timu ya Zesco ya nchini Zambia, aliyekanayo kwa misimu ya 2014, 2015 na 2016 kama kocha wa Zambia, akitokea timu aliyokaa sana ya Green Buffaloes 2002 – 2009.

Akiwa Zesco alichukua kombe la ligi kuu nchini Zambia 2014, 2015, kisha Barclay Cup 2014 tu, hapo klabu ya Yanga wakamuona na kumuhita kama kocha bora zaidi ya Plujin, sijui kama “Vetting & Scouting” ilifanyika sawa sawa na watu wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi hiyo, au mahaba ndio yalisukuma kumleta Yanga.

Ukiona mafaniko yake huko Zesco, yalitokana na matokeo ya vijana wa kazi pesa baadaye walikokuwa kwenye timu hiyo, waliyojituma sana kwa kasi kubwa wakati wote alipokuwepo kwenye Timu hiyo.

Leo mnamuona akibadili timu ya Yanga kwa muda mfupi, namuona Yondani anamcheza kama mchezesha timu dimba la kwanza, Oscar alicheza kama mshambuliaji na vituko vingi kutoka kwake hasa “sub” zake zisizobadili hali ya mchezo, siku ya Simba akumchezesha Bossuo kisa cha mchezaji kutokaa kambi kwa kuwaelewesha kuwa kambi ya timu inawekwa siku moja kabla ya mechi, amekua ni kocha asiyeleta matokeo.

Kwa maono ya ndoto chungu anatakiwa kusajili upya wachezaji kwani timu imekuwa na wachezaji hao hao muda sana au kuacha klabu hii ya Yanga, nadhani ndio watapata matokeo sahihi kwa wanayanga.

Pia mshahara wake ni mkubwa sana kutokana na mapato ya klabu wa Million 17 na akishinda kila mechi upewa Million 01, basi ni muhimu kuwa na watu wanoweza kusajili makocha kwa kuangalia vyanzo sahihi vywa klabu.

YANGA SC

Klabu ya Yanga yenye masikani yake Jijini Dar es Salaam, iliyoanzishwa miaka ya 1935 ni aibu kuwa klabu yenye mfumo wa kitaasisi unaofanyakazi kimtu binafsi kuliko mfumo taasisi.

Yanga ina Mwenyekiti wake Yusuph Manji, kwa jicho la nne ndio Bwana Fedha (Mhasibu), afisa biashara na afisa mwaajiri wa klabu, Yanga hii ina Katibu Mkuu, Afisa Habari, Mabaraza ya Vijana na Wazee, pamoja na wajumbe wa kamati kuu wasiokuwa na majukumu sahihi kiuhalisi ingawa katiba inawapa majukumu yakufanya, ukiitazama kwa juu ni klabu hisiyokuwa na mfumo sahihi wa kitaasisi kabisa.

Yanga inawachama wanaotamani kula chakula kila wakati (motokeo mazuri), lakini kupigania mifumo ya utafutaji chakula (Taasisi) hawana muda kabisa, ina wanachama, wadau na wapenzi wanaoamini katika mtu moja tu kila siku wakiamini yeye ni ndio taasisi.

Hapo majuzi mtu huyo amekumbwa na matatizo, Yanga sasa inalialia tu kila sehemu, haina pesa kabisa za kujiendesha, watumishi na wachezaji hawajalipwa mishahara miwili mpaka leo ingawa viongozi wanadai wamelipwa, wachezaji kama Bossuo alijitibu kwa pesa yake wakati anaumwa, kwa ufupi hakuna mfumo Taasisi kuna mfumo mahaba.

Natamani kuona Yanga Taasisi yenye Mkutano Mkuu wa wanachama huru, Bodi ya Wadhamini, Ofisi kuu yenye Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu makini, mwenye taaluma ya mpira na sio mapenzi na Yanga kama Dkt Tiboloa, yenye Idara mbalimbali kama Uzalishaji (Ufundi, Kiwanja, Mechi, Usajili na Michezo), Idara ya Masoko (Mauzo, Biashara, Wadhamini, Tiketi, Nyaraka na Vifaa vywa Yanga), Idara ya Utawala (Ajira, Habari na Mawasiliano, Ulinzi na Usalama, Mabunsa, IT, Jamii, Wanachama n.k) na Idara ya Fedha (Sera, Mipango, Uhasibu, Uwekezaji, Vitabu, Vywanzo vywa Mapato, na Ununuzi na Stoo), pamoja na kamati mbalimbali, kisha mabaraza muhimu kama ya wazee, wamama na vijana, na wafanyakazi sahihi kila sehemu, huku wakiwa na wadhamini wengi kila siku na mechi mbalimbali.

Tuangalie klabu kama Al Ahly Sporting Club (Red Devils) ya nchini Misri, yenye muundo sawa kabisa na Yanga hii.

Klabu hii ipo chini ya Mahmoud Faher wenye maono ya mpira na bishara kwenye klabu kama Mwenyekiti sawa na Manji wa Yanga, klabu ina idara nyingi sana kama Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikabu, Kuogelea, Karate na kadha wa kadha, kila idara ina Mkurugenzi akiwa chini ya Mkurugenzi Mkuu kama Mtendaji Mkuu wa Klabu, huku Timu ya Mpira ikiwa na Meneja, Kocha Mkuu na Makocha baadhi wasaidizi wanne, Daktari na wafanyakazi wengine kwenye maeneo mengi ya kiutendaji, wana uwanja wao wa Mokhtar El-Tetsh, lakini Yanga uwanja wao umeanguka tu ukuta mpaka leo ni shida kurudisha.

Mpaka leo klabu hii inawadhamini 11 kama Moro, Vodafone, Dominos, Coca Cola, Shell Helix, Huawei, Egyptian Steel, SaiBank, Nostles, Domty na Uber pamoja na Tez Tour, na hawa wote umwaga mipesa kwa klabu.

Hawa wadhamini wote ni utekelezaji wa timu kuwa Taasisi, lakini Yanga ina mdhamini moja tu ambaye ni kampuni ya mwenyekiti mtukufu, imeacha kuwa taasisi itakuyovuta watu na makampuni kuingia kuwadhamini kupitia idara ya biashara.

Wakati wa Simba na Yanga wanashindwa kuuza tu ata jezi, skafu na mambo kadha kwa wadau, wanaumiza sana hawa watu kupitia mashabiki maandazi ambao leo wanataka tuchangie timu kwa mpesa.

MANJI

Ni Mwenyekiti wa Yanga mwenye ushawishi mkubwa sana kwa wanachama na mashabiki wa Klabu hii, yani uwezi kuwambia kitu chochote juu ya Manji kati ya wanachama 8 kwenye kundi la watu 10.

Wanaamini na kujua bila Manji, Yanga itakufa na kuwa butu wanapenda matokeo ya uwanjani hawana muda na njia zipi za maboroshe ya klabu kusonga mbele kimapato na maendeleo, wao kila siku ni matokeo tu.

Mambo yote wamemuachia Mwenyekiti, sasa amekutwa na matatizo ya kiserikali yanoamkumba mpaka leo, tunaona klabu inayumba kimapato na kiutendaji hasa mishahara.

Tunaweza kujifunza kitu juu ya wale waliopigana sana ndani ya Yanga kuweka klabu kuwa Yanga Taasisi, leo hii timu ingekuwa haina shida ya mapato na utendaji, kwani mapato ya klabu yoyote ni wadhamini, wadau, kiingilio, ada za wanachama, baashara za vifaa vywa timu, uwekezaji kwenye majengo, hisa na chapa kimasoko.

Tazama Mwenyekiti wa Al Ahly klabu kafanya timu yake kuwa Taasisi kubwa sana, mpaka leo inamafanikio makubwa nje ya uwanja na ndani ya uwanja nani klabu ya pili duniani kimafanikio uwanjani baada ya Barcelona.

WANACHAMA WA YANGA

Hawa siwasemei leo wanachangamoto sana, wao wanataka matokeo tu kwenye mechi zote.

Wadau na wapenzi wa klabu wapo wanaotambua umuhimu wa klabu kuwa taasisi, lakini wanapata changamoto kwa wengi wanaoamini mfumo mtu na mnaweza pigana kabisa wakati mkieleweshana.

Wanachama ndio wanaosajili na kufukuza kwa mahaba yao, hakuna Idara ya usajili kabisa kwenye klabu.

Wanachama hawa wanasahau wakati wa Yanga na Simba, timu ilikwenda Uturuki au Zanzibar, lakin sasa timu imekwenda Kimbiji ambapo kutoka Makao Makuu mpaka huko Tsh1000 haipiti.

Wanachama hawa wanaosomewaga taarifa ya mapato na matumizi ya Yanga isiyokuwa na “Note of Accounts” na ushangilia kila wakati.

Wanachama hawa sasa wanasema wachangishane waokoe klabu, wanasema Lwandamina haondoke hasa mechi ya juzi lakini wao ndio walisema aje kwa kasi.

Wanachana hawa walimhita Zulu lama mkata umeme, sasa wanamhita Luku imekata.

NINI KIFANYIKE SASA?

Katibu Mkuu Boniface Mkwasa aitishe mkutano mkuu kwa mamlaka ya kikatiba kupitia mwenyekiti huko alipo, aseme na wanachama na wadau wa Yanga waweze kuchangia ata Tsh 5000 na kuendelea nchi nzima, hakika watapata pesa nyingi na kurudisha imani kwa wachezaji na mambo mengi yataenda kwa kasi pale Jangwani.

Pia kila tawi la Yanga kuchangia Tsh 200,000 kwa tawi dogo na kubwa mpaka 1,000,000 kwa kuokoa timu.

Pili wapunguze mishahara ya watu hasa watumishi, wachezaji na matumizi ya kambi za muda mrefu na matumizi yasio ya lazima kwenye klabu.

Tatu watengeneze mfumo kazi kwenye klabu na sio mtu.

Nne wapunguze watu wanaozaga tu muda wote pale makao makuu ya klabu, kuweka huru wa makampuni, watu makini na wapenzi wa klabu kuwaona kwa msaada na mawazo wakati wa kazi.

Mwisho waanzishe Idara ya Masoko kwa kasi ya kutafuta wadau makini, wadhamini na vyanzo vipya vywa kuuza Yanga kama chapa kwa umma wa kitanzania na nje.

Fikra huru sio ndoto mpurulano, Zambia wanaenda na ndege kwa jicho mahaba, ni muhimu kuwa wakweli hili kuwapa fulaha kila wakati wanachama, wadau na wapenzi wa Yanga SC wakimataifa.

Mwisho!

0715 011 406

(78)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available