Fredy Masolwa MICHEZO

Cheche la Jumapili;- SAAD KAWEMBA Kashindwa Kuongoza Azam Fc sasa??

Saad Kawemba, CEO Azam FC

Na. Fredy Masolwa.

Jumamosi ya tarehe 01/04/2017 kuanzia saa 10 jioni, nilipata tazama mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), kati ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) “Wakimataifa” wa Jangwani na Azam Football Club “Rambaramba” wa Chamanzi, kwenye uwanja wa Taifa Jijini, Dar es Salaam.

Kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo mpaka kipindi cha pili kabla ya Yanga kufunga goli la kuongoza, wapenzi, wadau na mashabiki wa Yanga waliishi bila amani, fulaha na msongo wa mawazo uliojaa mtikisiko ya moyo pande zote za miili yao.

Azam FC walishambulia kila wakati lango la Yanga kwa pande zote za uwanja, walitamba katikati kwa kuweka viungo wazuri na wengi kuliko Yanga, nyuma walijipanga vizuri kwa ukuta imara uliompa shida Obrey Chirwa kutamba maeneo hayo, huku mbele wakimuweka mshambuliaji wao hatari Yahaya Mohammed “Mkazuzu”, aliyesumbua sana mabeki wa Yanga wakati wote, kwa ufupi Azam FC waliwapa Presha sana timu ya Yanga iliyokuwa na kikosi hafifu nje na kikosi chake kikuu, kwa mchezo safi sana.

Mpira ulimalizika salama kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1 toka kwa Chirwa, licha ya Azam FC kucheza soka zuri kwa vipindi vyote na kutengeneza nafasi nyingi sana za kufunga mabao.

Pia jana tarehe 29/04/2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salam, walicheza na Simba SC mechi ya kombe la FA (ASFC), kwa ukweli Azam walikuwa hawana namna ya kushinda kutokana na mfumo wetu wa mpira Tanzania.

Walitolewa kwenye mikakati yao ya ushindi na mchezo huo kwenye dakika ya 07 nadhani, baada ya kupewa kadi nyekundu kwa mchezaji wao wa kutumainiwa katikati Sure Boy, sasa Azam naona wakishindwa kucheza nje ya uwanja kama zamani.

Je Kawemba hawezi au hajui kucheza nje ya uwanja kwa mpira au mfumo wa mpira wetu Tanzania?

Je Kawemba ndani ataweza lini kwa Azam nyenye kila kitu?

Je nini kinamshinda kushinda ndani na nje?

Mechi ya Simba na Azam ilimalizika kwa Simba kushinda kwa goli moja, Simba wamesonga mbele kwenye Fainali hiyo wakisubiri mshindi kati ya Mbao na Yanga leo.

Nikajiuliza swali kwanini Azam hawafanyi vizuri muda mrefu, licha ya kuwa na kila kitu cha mpira wa miguu?

Na kupata maswali mengi badala ya majibu ya swali langu, yasiokuwa na majibu chanya kwa wapenzi wa mpira nchini!

AZAM FC

Ilianza mnamo tarehe 24/06/2007 huko Pugu Kajiungeni na kuamia Chamanzi nje kidogo mwajiji la raha, Dar es Salaam, iliyoanzishwa na kumilikiwa mpaka sasa na tajiri wa Tanzania Said Bakhresa, klabu yenye masikani yake ya kudumu huko Chamanzi, wakiwa na Uwanja wao wa Azam Complex uliyowekewa kila kitu cha mchezo wa mpira wa miguu.

Sasa ikiongozwa na Abubakar Bakhresa kama Mwenyekiti wa Timu, huku Mtendaji Mkuu (CEO) wake akiwa ni ndugu Saad Kawemba kama injini ya timu kwa shughuli za kila siku kwa timu.

Azam ina wachezaji wenye uraia wa Tanzania na nje ya nchi, sasa ikinolewa na Kocha Mkuu mpya “mzungu” Aristica Cioaba mwenye uwezo mkubwa wa kufundisha, kwa mujibu wa Kawemba lakini matokeo yake sio mazuri mpaka leo.

Ukiangali timu tangu ingie kwenye ligi kuu msimu wa 2008/2009, imeweza kuchukua ubigwa mara moja tu msimu wa 2013/2014 licha ya kuwa na kila kitu cha mpira wa miguu tofauti na Simba, Yanga na timu zingine za Ligi Kuu Bara, msimu wa 2009/2010 ilikuwa nafasi ya 3 na 2010/2011 ilikuwa nafasi ya 3, msimu wa 2011/2012 nafasi ya 2, msimu wa 2012/2013 nafasi ya 3, na 2015/2016 nafasi ya 2, huku 2015 ikishinda Kombe la Kagame.

Mpaka sasa kwa miaka 10 imefundishwa na makocha 7, bila mafaniko chanya kwenye mchezo wa soka nchini na Afrika, 2008/2009 timu imefundishwa na Neider Dos Santos mzungu huyu kama Kocha Mkuu, 2009/2010 Itamar Anorin mzungu pia, 2010 – 2012 na 2015 – 05/2016 Stewart Hall mzungu, 2012 Bons Bunjak mzungu, 2013/2014 Josep Omog (kocha wa Klabu ya Simba sasa), na aliyeondolewa hivi karibuni Zeben Herbandez mwezi wa 06, 2016 alipoingia mpaka mwezi 12, 2016 na kuletwa Cioaba.

Hii ndio klabu ya Azam ina kila aina ya akili, hekima na busara za kutumia maliasili zake kuwa bora barani Afrika, lakini inakuwa sio bora kwa mwendo wa kiutendaji unaotazama akili za Yanga na Simba kupitia makaratasi na vijiwe soka na siasa, kuliko mpira wa kiufundi, kibiashara na uwanjani.

SAAD KAWEMBA

Huyu ni Mtendaji Mkuu wa Azam FC tangu mwaka 2014, akitokea shirikisho la soka Tanzania (TFF) kama Mkurugenzi wa Mashindano.

Bodi ya Wakurugenzi wa Azam FC, imempa jukumu la kusimamia timu hiyo kwa hatua zote za kila siku, ana ofisi yenye watendaji kwa kila idara na washauri mbalimbali wenye uwezo mkubwa kimpira na kiutawala.

Je anawatumia watendaji hao na washauri vizuri?

Je ni mfumo upi wa kiutendaji au uongozi anaoutumia kuongoza Azam FC?

Je anauwezo wa kutoa pesa yoyote benki kwa matumizi ya Azam FC?

Je ni mtendaji mkuu, kiongozi mkuu au mtawala mkuu kwenye timu ya Azam FC?

Je ana uwezo wa kuongoza timu kubwa kama Azam FC, aliozaliwa nao! Au kusomea?!!

Je anajua mpira wa miguu kwa mfumo wa kibiashara au uwanjani?

Maswali ni mengi sana na majibu ni machache sana, bwana Saad Kawemba ni kijana mtanashati, mwenye muonekano mzuri, anaongea vizuri na utendaji wake ni mzuri kwa muonekano, lakini kwa maono yangu wakati nikiwa nimenyeshewa na mvua ya Dar es Salaam jana, iliyonifanya kusombwa na maji kwenye daraja la Jangwani na kuokolewa mitaa ya Hananasif, basi nasema hafai kuendelea kuongoza Azam Football Club kama Mtendaji Mkuu sasa labda kama Afisa Habari, kwasababu nyingi za kushindwa kuweka mfumo wa kugawanya majukumu ya uzalishaji wa timu (Ofisi, Usajili, Uwanjani na Michezo) kikamilifu kwenye uongozi wake Azam FC.

LIGI KUU VPL & FA

Ukiitazama Azam FC kwenye Ligi Kuu Bara, sasa ipo kwenye nafasi ya 03, ikicheza michezo 27 wakinyakuwa pointi 46, nyuma ya zaidi ya pointi 10 za Yanga na Simba wanaoshika nafasi ya 1 na 2 kwenye Ligi.

Wanamichezo 03 waliobakiza kucheza dhidi ya Toto African, Mbao FC na Kagera Sugar mechi zote akicheza Chamanzi Azam Complex, mpaka sasa wakishinda michezo 12, kufungwa 05 na kutoka sare 10 wakiwa na magoli 31, kwa hali hii haiwezekani kuwa bigwa wa VPL 2016/2017.

Huku kombe la FA wakitolewa jana na Simba SC, kwa kufungwa goli moja.

WACHEZAJI NA UFUNDI

Ukitazama wachezaji wao kiufundi kwenye klabu ya Azam, kuna ukakasi mkubwa sana wa aina ya wachezaji wanaotoka nje ya nchini, bora wazawa kwa ubora.

Uwezo wao ni wakawaida sana, wanalipwa mipesa na stahiki nyingi sana lakini hakuna kitu, nikawa najiuliza au wananuliwa Tsh 3 lakini ofisi inasema Tsh 1000 hizo 997 zinapotea.

Mwanafunzi akifundishwa na Walimu wengi kidato cha kwanza tu, kuelewa kwake ni vigumu sana mpaka sasa Azam imefundishwa na makocha wengi sana.

Kwenye Idara ya Ufundi ina wataalamu waliosoma makaratasi darasani na sio waliosoma mpira wa Tanzania, hili ni tatizo kubwa.

SHIDA NI NINI AZAM?

Shida ya kwanza ni Mtendaji Mkuu labda?

Huyu ndio wenye nguvu na uwezo wa kupanga watendaji, uwajibikaji na majukumu ya kila mtu wa ofisini, uwanjani, ufundi na miundombinu.

Huyu ndio anaanza kutafuta mali ghafi (kocha na wachezaji), anawapeleka kwa mashine ya uzalishaji (Idara ya Ufundi na Uwanjani), huku yeye akisimamia uzalishaji huo kwenye mashine, mwisho anatoa mali kamili (mchezaji mzuri kwa Azam na wakuuzika sehemu nyingine), itakayo uzika vizuri kwa wateja (mashabiki) na wadau (timu kubwa nyingine) na kuwapa fulaha walaji kila wakati (ushindi na magoli).

Kawemba kashindwa sasa??!!, kwani Azam FC wanakila kitu cha mpira wa miguu, kama uwanja wa kufanyia mazoezi na mechi mbalimbali, wana rasilimali fedha na watu wenye ujuzi mbalimbali, wadhamini wenye majina na wanaowamwagia mipesa kibao kwao kama NMB, Vodacom, Azam TV, DTB Bank, Selcom, Bakhresa Group of Companies na wadu wengine wengu, pia ina kila kitu na kitendea kazi cha mchezo wa mpira wa miguu, timu inauwezo ata wa kumchukua mchezaji yoyote duniani kama Sadio Mane wa Liverpool, na ata uwezo wa kumchukua kocha yoyote kokote alipo, kwani mwaka wa fedha wa 2016/2017 imeidhinishiwa bajeti ya zaidi ya billion 57 na bodi ya wakurugenzi ya Azam FC.

Ukitazama Azam FC haina utofauti sana na Tout Puissait Mazembe (TP Mazembe) ya nchini Congo, chini ya Meneja wake Gabriel Erivalcho kama Mtendaji Mkuu wa Timu wenye uwezo sawa na Kawemba, lakini timu yake inamafaniko makubwa sana kiofisini, uwanjani kimatokeo na ufundi.

Mpira wa miguu ni mchanyato wa kazi na majukumu mbalimbali ya ofisini, uwanjani na ufundi kwa kugawana majukumu. Ingawa nimeelezwa huko Azam FC mgawanyo wa majukumu ni changamoto sijui ni kweli!!??.

Azam FC wajitafakari sasa, ingawa mmiliki wake upenda sana michezo za mbio za magari, huku kwenye mpira anafanya kama fulaha tu na kuwaumiza wapenzi wa Timu hii ya Azam FC!

Azam FC inatakiwa kuongoza Ligi VPL na FA kwa miaka yote kwa jinsi ilivyo, lakini sasa ni tofauti!!

Tafakari chukua hatua!!!!
Haki ya Elimu!!!!

Mwisho!

0715 011 406

(66)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available