ELIMU SAYANSI & TEKNOLOJIA

Waliofaulu Darasa la Saba Lazima Waendelee na Masomo – Majaliwa

Na Sabina Wandiba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana
waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya kutosha.

“Serikali haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato cha kwanza.

Halmashauri zilijua tangu mapema wanafunzi wanaenda shule za msingi, kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari kwa asilimia 100,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Lindi, baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo Ikulu ndogo wilayani Nachingwea.

Waziri Mkuu aliwasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka.

Alisema Serikali ya awamu ya tano, imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari.

“Tumesema elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati azma ya Serikali ni kutoa elimu ya bure. Hakikisheni wote wanaingia katika chaguo la kwanza,” amesema.

Aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ambazo zimefaulisha wanafunzi, lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha warudi mezani na kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapangwa na kuanza na wenzao katika chaguo la kwanza kwani wakisubiri chaguo la pili watachelewa.

(62)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available