SIASA TANZANIA

Zuma Awagomea ANC; Bunge Kujaribu Kumuondoa Kesho

(PICHA NA AFP / MUJAHID SAFODIEN

Na. M. M. Mwanakijiji

Rais wa Afrika ya Kusini anayekabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka ajiuzulu Bw. Jacob Zuma (75) amegoma kuachia madaraka kama alivyotakiwa kufanya hivyo na chama chake cha ANC. Siku ya Jumanne Kamati Kuu ya ANC ilimpatia masaa arobaini na nane aachie ngazi ama sivyo kingechukua hatua dhidi yake ya kumuondoa kwenye Urais.

Mvutano mkubwa unaendelea kati ya kambi inayomuunga mkono Bw. Zuma na kambi inayojionesha kuwa ni ya mabadiliko ndani ya  chama hicho kufuatia kuchaguliwa kwa Bw. Cyril Ramaphosa kuwa Mwenyekiti mpya wa ANC. Zuma amezungumza leo na waandishi wa habari na kusema kuwa ANC haijamtendea haki na wala kumpatia sababu ya wao kumtaka ajiuzulu nafasi yake ya Urais. Zuma anatarajiwa kuzungumza tena baadaye leo.

Wakati huo huo jeshi la polisi limeendelea kufanya uchunguzi na kuendesha upelelezi baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuripoti kuwa Jeshi hilo limevamia sehemu mbalimbali na kuchukua vitu mbalimbali kwa ajili ya ushahidi.

Kwa upande wake kufuatia kugoma kwa Zuma kujiuzulu chama cha ANC kimepanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Bungeni kesho na hivyo kumuondoa madarakani Zuma kama kura hiyo itapita Mara baada ya kura hiyo kupigwa kama itafanikiwa inavyotarajiwa basi Bw. Cyril Ramaphosa ataapisha kama Rais mpya wa nchi hiyo.

(50)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available