KIMATAIFA SIASA TANZANIA

Raila Apewa Ruhusa Kuangalia Kompyuta za Tume ya Uchaguzi

Na. M. M. Mwanakijiji

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha NASA cha Kenya Bw. Raila Odinga amepata ushindi mdogo katika Mahakama Kuu ya Kenya baada ya mahakama hiyo kumruhusu kuangalia mitandao na kompyuta za tume ya uchaguzi ambazo zilitumika katika kukusanya na kuchambua matokeo na hatimaye kuyatangaza kwa wananchi.

Mahakama hiyo leo Jumatatu imetoa ushindi huo ili kujibu mojawapo ya hoja zilizotolewa na muungano huo wa vyama vya upinzani wa NASA ambao ulidai kuwa kulikuwa na majaribio ya kuvuruga mtandao huo na uwezekano wa kubadilisha matokeo. Hadi hivi sasa fomu mbalimbali ambazo zilitumika kwenye uchaguzi huo uliofanyika wiki mbili hizi zilizopita bado hazijawekwa kwenye mtandao huo na kumekuwa na madai kuwa mtandao huo bado unatoa matokeo ambayo yanapingana na yale yaliyotangazwa majimboni.

Endapo itaonekana kwa namna yoyote ile taarifa ambazo zipo kwenye mitandao hiyo zitaonekana kuzua mjadala kwa kuwa na tofauti au kuonesha kuwa zilidukuliwa kwa namna yoyote inaweza kulazimisha kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya kama Mahakama Kuu itaona hivyo. Uchaguzi Mkuu utarudiwa ndani ya siku sitini. Lakini kama mahakama itaona hakuna sababu ya msingi ya kubatilisha matokeo basi itathibitisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyata wa chama cha Jubilee na hivyo kuruhusu kuapishwa kwake.

(101)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available