SIASA TANZANIA

Magufuli Asikiliza Maoni ya Watanzania; Apangua Wizara; Katibu Mpya wa Bunge!

Rais Magufuli akitangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri leo. Picha na Ikulu.

Na. Sabina Wandiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri huku akitilia maanani maoni ya Watanzania mbalimbali ya kutaka weledi na ufanisi katika baadhi ya wizara hizo.

Mojawapo ya mambo ambayo Rais Magufuli ameyafanya na ambayo yamekuwa yakiombwa mara kwa mara ni lile la kutenganisha Wizara ya Nishati na Madini na kuzifanya kuwa wizara mbili huru. Baada ya kuondolewa kwa Sospeter Muhongo toka Wizara hiyo, wizara ilibakia bila waziri hadi leo ambapo baada ya kutenganishwa kila wizara imepata waziri wake na hivyo kuhakikisha tatizo la sekta moja halitoweza kuwa tatizo la sekta nyingine pale inapotokea Waziri hayupo.

Wizara ya Nishati sasa inaenda kuongozwa na Medard Kalemani wakati Wizara ya Madini inaenda kuongozwa na Angela Kairuki.

Pamoja na jambo hilo Rais Magufuli pia amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambayo amekuwa akilalamikiwa kwa muda mrefu Profesa Jumanne Maghembe. Wizara hiyo sasa inaenda kuongozwa na Dkt. Hamisi Kigwangala ambaye alikuwa ni Naibu Waziri wa Afya chini ya Ummy Mwalimu na naibu wake atakuwa Ngailonga Josephat Hashunga (CCM Vwawa).

Wizara ya Tamisemi ambayo ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais sasa imepatiwa waziri wake ambaye ni Selemani Jafo. George Mkuchika ambaye aliwahi kuwa waziri huko nyuma amerudishwa ndani ya wizara hiyo na moja kwa moja kuingia ofisi ya Rais ambapo anaenda kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. George Mkuchika. Wizara hiyo pia inasimamia Idara ya Usalama wa Taifa.

Mojawapo ya teuzi ambazo hazikutarajiwa ni za Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mbozi Bi. Juliana Shonza kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ambayo inaendea kuongozwa na Harrison Mwakyembe.

Katika mabadiliko haya idadi ya wizara imeongezeka kutoka 19 hadi 21 na idadi ya manaibu waziri kutoka 16 hadi 21.

Orodha kamili ya Baraza la mawaziri lilivyo sasa na kama wateuliwa wote watakubali teuzi zao na kuapishwa Jumatatu asubuhi ni kama ifuatavyo kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu.

 

01. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

I. Waziri – George Huruma Mkuchika

02. Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

I. Waziri – Selemani Said Jafo

II. Naibu Waziri – Joseph Sinkamba Kandege

III. Naibu Wazri – George Joseph Kakunda

03. Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

I. Waziri – January Yusuf Makamba

II. Naibu Waziri – Kangi Alphaxard Lugola

04. Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.

I. Waziri – Jenista Joackim Mhagama

II. Naibu Waziri – Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)

III. Naibu Waziri – Stella Alex Ikupa (Walemavu)

05. Wizara ya Kilimo.

I. Waziri – Dkt. Charles John Tizeba

II. Naibu Waziri – Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa

06. Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

I. Waziri – Luhaga Joelson Mpina

II. Naibu Waziri – Abdallah Hamis Ulega

07. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

I. Waziri – Prof. Makame Mbarawa Mnyaa

II. Naibu Waziri – Mhandisi Atashasta Justus Nditiye

III. Naibu Waziri – Elias John Kwandikwa

08. Wizara ya Fedha na Mipango.

I. Waziri – Dkt. Philip Isdor Mpango

II. Naibu Waziri – Dkt. Ashatu Kijaji

09. Wizara ya Nishati.
I. Waziri – Dkt. Medard Matogoro Kalemani

II. Naibu Waziri – Subira Hamis Mgalu

10. Wizara ya Madini.

I. Waziri – Angellah Kairuki

II. Naibu Waziri – Stanslaus Haroon Nyongo

11. Wizara ya Katiba na Sheria.
I. Waziri – Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko
Kabudi.

12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

I. Waziri – Dkt. Augustine Philip Mahiga

II. Naibu Waziri – Dkt. Susan Alphonce Kolimba

13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).

I. Waziri – Dkt. Hussein Ali Mwinyi

14. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

I. Waziri – Mwigulu Lameck Nchemba

II. Naibu Waziri – Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

15. Wizara ya Maliasili na Utalii.

I. Waziri – Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla

II. Naibu Waziri – Josephat Ngailonga Hasunga

16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

I. Waziri – William Vangimembe Lukuvi

II. Naibu Waziri – Angelina Sylivester Mabula

17. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

I. Waziri – Charles Paul Mwijage

II. Naibu Waziri – Mhandisi Stella Martin Manyanya

18. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

I. Waziri – Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

II. Naibu Waziri – William Tate Ole Nasha

19. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

I. Waziri – Ummy Ally Mwalimu

II. Naibu Waziri – Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile

20. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

I. Waziri – Dkt. Harrison George Mwakyembe

II. Naibu Waziri – Juliana Daniel Shonza

21. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

I. Waziri – Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe

II. Naibu Waziri – Jumaa Hamidu Aweso

Pamoja na mabadiliko hayo Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa Katibu wa Bunge ambapo amemuondoa Dkt. Thomas Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine na nafasi yake kujazwa na Stephen Kagaigai. Kabla ya uteuzi wake Kagaigai alikuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri.

Kuondolewa kwa Kashilila kumepokelewa na baadhi ya watu ambao hawakuwa wanajua madaraka ya Rais kumteua Katibu wa Bunge ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Utumishi wa Bunge.

(191)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available