SIASA TANZANIA

Jenerali Semfuko Apongeza Makampuni ya Utalii Yanavyoshiriki Katika Hifadhi ya Mbuga na Wanyamapori

Gen. Hamis Semfuko akiwa na wajumbe wa bodi, wafanyakazi wa hifadhi, waandishi wa habari na watendaji wa makampuni ya kitalii kwenye ziara yake huko Maswa. Kulia kwa Gen. Semfuko ni Lt Generali Mstaafu Samuel Ndomba, mjumbe wa Bodi.

WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori la Akiba la Maswa linanalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali  (mstaafu) Hamisi Semfuko alipokuwa akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo. “La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike,” alisema Semfuko.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu. Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris (TGTS).

Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ilitoa ufadhili mbalimnbali ikiwemo fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi inayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine ya hifadhi.

Katika ziara hiyo TAWA imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dkt.James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa  makampuni ya uwindaji wa kitalii yaliyowekeza katika maeneo yao.

Maeneo yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Limited. Dk Wakibara alisema, licha  mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo  ya kampuni hizo imekuwa ikitoa  takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji na halmashauri ambapo wawekezaji hao wanafanya kazi.

Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159  vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini kote. “Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA”alisema

Alisema kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia dola milioni 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi kufikia dola milioni 80. “Kuna dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo  kiwango cha kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya kimataifa”alisema Dkt. Wakibara.

Mwenyekiti wa bodi ya TAWA, Meja Jenerali Hamisi Semfuko alisema mamlaka hiyo ipo katika mabadiliko  makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya maji, afya Elimu na uhifadhi.

(57)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available