Rais Magufuli amteua Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani

 

Paul Mpazi (Zama Mpya)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mawaziri walioteuliwa katika mabadiliko haya wataapishwa Jumatatu tarehe 13 Juni, 2016 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

About the author

Paul Mpazi

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available