MAISHA SAYANSI & TEKNOLOJIA

Prof. Mbarawa Atoa Onyo kwa Madereva wa Malori Wanaoharibu Barabara.

Na Sabina Wandiba.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wa malori ya mchanga na kokoto watakaobainika kutofuata sheria za ubebaji wa bidhaa hiyo na hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma katika ziara yake ya kukagua barabara ya Kidahwe-Kasulu yenye urefu wa kilometa 50 ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya barabara kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla hivyo haita mvumilia mtu yeyote atakayebainika kuharibu miundombu hiy kwa makusudi.

“Kuanzia sasa Serikali haitavumilia madereva wasiozingatia kanuni na sheria za usafirishaji wa mizigo katika barabara nchini, hivyo nawaagiza Mameneja wa TANROADS katika mikoa yote nchini kusimamia sheria ili kudhibiti miundombinu ya barabara, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameliomba Jeshi la Polisi kushirikiana vema na makandarasi wanaojenga miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwachukulia hatua za
kisheria baadhi ya watu wasio waaminifu ambao wanaiba vifaa vya makandarasi jambo linalochangia kukwamisha shughuli za ujenzi wa barabara.

Amewataka wananchi wa Wilaya ya Kasulu kutoa ushirikiano kwa mkandarasi wa kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara hiyo ili kuwezesha ujenzi huo kukamilika haraka.

Naye Meneja wa TANROADS mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma, amebainisha changamoto zinazokabili mradi huo kuwa ni wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi hali inayosababisha mradi kusuasua.

“Wananachi tambueni kuwa fedha hizi ni za kwenu mnapohujumu vifaa vya ujenzi ni dhahiri mnajicheleweshea maendeleo na kukwamisha fursa za kiuchumi katika wilaya yenu”, amesema Eng. Choma.

Kwa upande wake Mhandisi Mkazi Mekbib Tesfaye anayesimamia mradi huo kutoka Kampuni ya DOCH Limited, amesema kuwa mradi huo umefikia asilimia 24 ambapo kwa sasa kazi inayofanyika ni ujenzi wa
madaraja mawili na makalvati katika barabara hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa ametembelea Chuo cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Mkoani Kigoma na kuahidi uongozi kuwa atazishughulikia haraka changamoto kadhaa zinazokikabili chuo
hicho ili kuweka mazingira rafiki ya kujisomea kwa wanafunzi wanaosomea taalauma hiyo.

“Nitahakikisha chuo hiki kinajengewa mabweni ya wanafunzi pamoja na kuongeza gari kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazofanyika hapa”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Peter Mlonganile wakati akisoma taaraifa ya chuo hicho kwa Waziri huyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo hayo kwa viwango vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuzitatua changamoto ndogo ndogo zinazo kikabili chuo hicho.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara, reli, uwanja wa ndege, katika mkoa wa Kigoma ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha miundombinu hiyo na kuuwezesha mkoa
kufanya biashara kirahisi na mikoa mingine ya Tanzania na nchi za Congo DRC, Rwanda na Burundi.

(18)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available