MAISHA TANZANIA

OZ Group’s Yawashika Mkono Wahanga wa Tetemeko la Bukoba

Mratibu Mkazi wa Kanda OZ Groups, Bi Diana Madukwa akiwa pamoja na Vijana wa Kituo cha Yatima - Bukoba

Na Diana J, Madukwa.

BUKOBA – Leo tarehe 7 Desemba 2016, kundi la Whatsapp la Operesheni Zinduka (OZ Group)  lililoanzishwa wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuendelea kudumu baada ya uchaguzi limekabidhi  msaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi, katika kituo cha watoto yatima kiitwacho “Ummuly Yatima Orphan Children Home” (UYACHO) kilichopo eneo la Hamugembe kwenye Manispaa ya Bukoba Mjini. Misaada hii ilitolewa moja kwa moja kwa wahanga badala ya kuipeleka kwa taasisi za serikali ili kuhakikisha misaada iliyotolewa na wanachama wa OZ inawafikia walengwa moja kwa moja na kuondoa ukiritimba wa kiserikali usio wa lazima.

Nyumba iliyobomoka kabisa na kufanya vijana kukosa sehemu sahihi ya kulala vizuri sasa.
Nyumba ya Kituo cha UYACHO iliyobomoka kabisa na kufanya vijana kukosa sehemu sahihi ya kulala vizuri sasa.

OZ Group’s ni Umoja wa watanzania wenye maono sawa katika fursa, jamii, maendeleo mbalimbali, taaluma na mambo mbalimbali ya kujenga nchi kupita mtandao wa “Whatapps”, iliwakilishwa Mratibu Mkazi wa Kanda Bi. Diana Madukwa  kwa kukabidhi vitu mbalimbali kwa vijana waliobakia kwenye kituo hicho.

Mratibu Mkazi wa OZ Groups, Bi. Diana Madukwa akikabidhi baadhi ya Vitu kwa Mama Mlezi wa Kituo.
Mratibu Mkazi wa Kanda OZ Groups, Bi. Diana Madukwa akikabidhi baadhi ya Vitu kwa Mama Mlezi wa Kituo Bi. Saada.
img-20161207-wa0054
Watoto wakiwa sehemu wanayolala kwa sasa na Bi. Diana.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni kama Nguo za watoto mpya, unga wa mahindi kilogram 100, Mafuta ya kupikia, Sabuni za miche katoni moja, Mchele, Sukari, Sabuni ya unga, Mafuta ya kupaka mwilini, Dawa ya meno  whitedent, Chumvi, na Miswaki  ya meno kwa vijana hawa.

Wasimamizi wa kituo hicho, Bibi Saada na Mr Kachwamba waliwashukuru sana wana Oz Groups wote, kwa walichotoa kuwasaidia watoto hawa Yatima, huku bibi Saada alisema “Mungu awabariki wote mliowakumbuka watoto hawa yatima na Mungu awabariki sana kwa majitoleo yenu” Pia watoto wenyewe walishukuru sana, huku wakisema watawaombea dua kwa  Mungu wote waliotoa kwaajili yao.

img-20161207-wa0074
Moja ya Nyumba ilivyo kwasasa baada ya tetemeko kutokea.

Jicho la ZAMA MPYA limeweza kuona changomo kubwa walizonazo vijana hawa, kwani hawana sehemu sahihi ya kulala, kusomea, kuweka vitu vywao na chumba sahihi cha kutunza vitu kwa kukwepa jua na mvua kwa sasa, wanahitaji sana msaada wa kijamii kwa sasa.

Twendeni Bukoba tukawasaidie wahanga kwa pamoja.

img-20161207-wa0077_________________________________________________________________________

Baadhi ya Mali zilizobaki kwenye Kituo cha UYACHO, baada ya Tetemeko kuaribu Kituo Hicho
Baadhi ya Mali zilizobaki kwenye Kituo cha UYACHO, baada ya Tetemeko kuaribu Kituo Hicho

Mwisho

(25)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available