MAISHA

Mrema Aishutumu Magereza Kuzuia Wafungwa Waliolipiwa Faini

Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt. Augustine Mrema akiongea na Waandishibwa Habari (hawapo pichani).

Na Sabina Wandiba

Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt. Augustine Mrema amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia Jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.

Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.

“Mimi nimeona nisinyamaze, Napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalo tatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi”?, alisema Mrema.

Amesema, amesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota.

“Mrema amefanya kosa lipi? ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.

(18)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available