MAISHA TANZANIA

Madaktari na Wauguzi 40 Toka Korea Kusini Watoa Tiba Bure Sengerema

Na. D. Madukwa

Na. D. Madukwa
SENGEREMA, MWANZA Jopo la madaktari na wauguzi 40 shirika la World mission frontier wakishirikiana na Asan Medical center kutoka kutoka Korea Kusini wamefika Tanzania katika wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, jopo hilo limetoa matibabu katika maeneo ya Isole na Katunguru wilayani Sengerema.
Zaidi ya watu 1400  kutoka maeneo mbalimbali ya Sengerema wamenufaika na matibabu hayo.
Matibabu hayo yametolewa bure kwa wagonjwa wote waliofika kupata huduma pia baadhi ya wagonjwa  wameweza kufanyiwa upasuaji na Daktari wa upasuaji Kim.
Diwani wa Kata ya Katunguru Bw. Mathew Lubongeja Ndalahwa amefurahishwa sana na kazi kubwa iliyofanywa na watu wa Korea kusini  na amewaomba waendelee na moyo huo huo wa kujitolea kwa kutoa matibabu bure kwa watanzania,.
Pia amewashukuru wananchi kwa  kujitokeza kwa wingi kuja kupata huduma hiyo ya kutatua matatizo mbalimbali ya afya zao amabyo mengine wamekuwa wakihangaika nayo kwa muda mrefu.
Madaktari na wauguzi wa Korea kusini kama vile: Dr Park Kyun, Dr Ra, Dr Kim, na manesi kama Kim Rahee,  Kim Hyunji na wengine wengi wanawashukuru sana Watanzania wa wilaya ya Sengerema kwa ushirikiano waliouonesha katika muda wa matibabu kwenye maeneo ya Isole na Katunguru (pichani).

(48)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available