MAISHA

LUKUVI Alia Na Mashamba Yasiyoendelezwa.

Na Dotto Kwilasa

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali imeshindwa kuyafutia hati miliki mashamba pori mengi ambayo hayajaendelezwa baada ya kubaini kuwa yamekopewa mabilioni ya fedha katika taasisi za kibenki hapa nchini.

Pia amezitahadharisha taasisi za kibenki nchini kuwa makini kwani endapo itatoa mkopo kwa dhamana ya shamba na likaleta mgogoro kwa kutoendelezwa watakula nao sahani moja.

Hayo aliyasema jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya serikali kuwasilisha taarifa ya ardhi kuhusu hatma ya matumizi ya mashamba makubwa yaliyotelekezwa.

Ni jukumu la serikali kuhakikisha linalinda umiliki halali kwa watu wenye hati miliki na si kuwanyang’anya mashamba kiholela”alisema Lukuvi.

Vile vile alisema kuwa, licha ya Rais kuwapa jukumu la kuhakikisha wanafuta mashamba yote yasiyoendelezwa, na kazi hiyo inaendelea lakini wanahakikisha wanafuata sheria ili wasije wakastakiwa.

Alisema wakati wanaendelea na utaratibu huo wa kufuta mashamba yasiyoendelezwa wamebaini kuwa kuna mashamba mengi ambayo yana mikopo katika taasisi za benki hivyo lazima wafuate taratibu ili benki 8 zisije kufilisika.

Waziri huyo alisema, katika mashamba hayo kuna yaliyochukuliwa mikopo nje ya nchi nayale yale 8 yachukuliwa mikopo ndani ya nchi na ordha yote wanayo wanaendeklea kuifanyia kazi kikamilifu.

 

Alisema wakati taasisi hizo za kibenki zikijigamba kwa kushiriki katika sekta ya kilimo, zimekuwa zikishindwa kuangalia uhalisia ikiwa ni pamoja na kufika katika mashamba hayo kuona kama yanaendelezwa.

Alibainisha kuwa mkakati wa wizara hiyo hivi sasa ni kukutana na taasisi za benki zote ambazo mashamba hayo yamekopea pesa, ili waweze kufanya mazingumzo na kuona namna bora ya kumaliza mgogoro huo.

“Kimsingi mikopo yote iliyokopewa benki kupitia mashamba hayo, imesajiliwa kwa msajili hivyo hatuwezi kukulupuka lazima tufuate sheria katika kufuta mashamba hayo ili tusije kuingia kwenywe matatizo na kubaki tukijilaumu,”alisema Lukuvi.

Alitolea mfano shamba moja ambalo limekopewa Dola za kimarekani, milioni 16 mara nane, ambapo utaona jinsi kulivyo na hali ya hatari na ugumu wa kazi hiyo, na kwamba kuna ulazima wa kuwa makini.

Lukuvi alisema, kwa bahati mbaya licha ya mikopo hiyo kukopwa kwa dhamana ya mashamba lakini haitumiki kwa manufaa ya kuwekeza kwenye mashamba bali inatumika kuwekeza katika biashara nyingine ikiwemo kujenga nyumba za kupangisha nje ya nchi.

Alisema, endapo ingekuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa basi sekta ya kilimo hapa nchi ingekuwa na mafanikio makubwa.

“Mashamba mengine ni vigumu kuyanyang’anya kutokana na hali hiyo,”alisema Lukuvi. Alisema, mabenki ambayo yatatoa mkopo kupitia mashamba ambayo hayajaenhdelezwa hayataonewa huruma yatachukuliwa hatua.

Alisema hawataacha watanzania wakiacha kunufaika na ardhi yao huku watu wajanja wakinunua ardhi kwa bei ndogo na kunufaisha. Kwa upande wake

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Atashasta Nditiye, aliitaka serikali kufatilia na kutoa maelekezo ya namna mashamba hayo yanavyopaswa kutumika kwani kumekuwa na migogoro mingi katika miji mikubwa kutokana na wananchi kujichukulia sheria mikononi.

Hata hivyo Lukuvi ameitaka serikali kutoa agizo la kisheria kwa kutoa mamlaka ya mipaka na ukubwa wa eneo ambalo wanapaswa kuhusika nalo watendaji wa vijiji kwani nao wamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro.
Mwisho

(39)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available