MAISHA

LAPF Yasaidia Kupunguza Tatizo La Maji.

Na Dotto Kwilasa

KUTOKANA na  changamoto ya ukosefu wa maji katika maeneo ya Ihumwa na Mtumba,Mfuko wa Pensheni wa wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umetoa hundi ya shilingi Milioni 6 kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Akikabidhi  hundi hiyo hivi karibuni mjini hapa, Meneja mawasiliano na masoko wa LAPF James Mlowe , kwa Mkurugenzi wa Manispaa (MD) Godwin Kunambi, Mlowe alisema mfuko huo umetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufufua visima vya maji vilivyoharibika na kuwasababishia wananchi usumbufu.

Hata hivyo Mlowe alisema mfuko huo ulipokea maombi kutoka katika ofisi ya Manispaa pamoja na ofisi ya mbunge wakiomba kupatiwa msaada wa kutengeneza visima vya maji katika kata ya Ihumwa na Mtumba kutokana na visima hivyo kuharibika na kuwasababishia usumbufu wa kukosea maji wakazi hao.

Alisema LAPF kama taasisi ya serikali imekuwa ikifanya shughuli nyingi na halmashauri mbalimbali nchini hususani shughuli za kimaendeleo.

“Kwa sasa Dodoma ni makao mkuu ya nchi hivyo kuna watu wengi wataamia hivyo hakuna sababu ya kuwepo na changamoto yoyote ya ukosefu wa maji”alisema.

Pia Mlowe alisema pesa zinazotolewa na taasisi mbalimbali pamoja na wahisani ni vyema zikatumiwa kwa majengo yaliyokusudiwa badala ya kuzibadilishia matumizi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma (MD) Edwin Kunambi amesema katika uongozi wake atahakikisha miradi yote iliyokusudiwa inafanyika kadri ilivyopangwa.

Mbali na hayo amesema watumishi waliopo chini ya uongozi wake ambao watafanya kazi kwa kukiuka utaratibu na kukiuka maadili watawajibishwa kwa mujibu wa taratibu za kazi na sheria.

“Ni kweli kwa sasa Dodoma kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji katika maeneo ambayo yapo nje ya mji,lakini kutokana na msaada ambao tumeupata kutoka LAPF, utasaidia kuboresha na kukarabati visima vya maji ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa maji”amesema Kunambi.

Kutokana na hatua hiyo ,diwani wa kata ya Mtumba Edward Maboje amesema ni jambo jema kwa kuwa wananchi watapata urahisi wa kupata maji na kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa sugu kwa vijiji vya mkoa huu.

Maboje alisema,msaada huo unelenga kufuta umaskini kutokana na kwamba wananchi wengi wanashindwa kufanya shughuli za uchumi kwa kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Mmoja wa wananchi waliozungumza na Gazeti hili juu ya msaada huo alisema kwake ni faraja kubwa kwao kwani wanapata adha kubwa ya upatikanaji wa maji ambapo wakati mwingine hupelekea kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na kufuata maji kwa umbali mrefu.

Mwisho.

(44)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available