KIMATAIFA TANZANIA

Zuma Apewa Masaa 48 Kujiuzulu au Atang’olewa

Na. Mwandishi Wetu

PRETORIA- AFRIKA YA KUSINI – Rais wa Afrika ya Kusini Bw. Jacob Zuma amepewa masaa 48  na chama chake cha African National Congress (ANC) kujiuzulu ama sivyo chama hicho kitatumia utaratibu wa kumpigia kura ya kumuondoa kwenye nafasi yake hiyo. Taarifa za masharti hayo zimekuja baada ya msafara wa Rais Mpya wa chama hicho Bw. Cyril Ramaphosa na katibu wake kuonekana ukielekea Ikulu ya Rais huyo.

Endapo Zuma atakubali kujiuzulu atakuwa ni rais wa pili wa Afrika katika miezi hii ya karibuni aliyelazimika kuondolewa madarakani kabla ya muda wake kuisha kufuatia shinikizo kutoka chama chake. Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alilazimika kuachia nafasi yake baada ya Jeshi la nchi yake pamoja na chama chake kuamua ajiuzulu nafasi zake zote.

Hadi hivi sasa haijajulikana kama Zuma atakuwa tayari kuachilia nafasi hiyo hasa kwa vile kwa muda mrefu sasa mashinikizo yote ya kumtaka ajiuzulu yaligonga mwamba. Kubwa ambalo tetesi zinaelezea kinaendelea ni namna gani anaweza kuachia ngazi bila kukabiliana na mashtaka ya ufisadi dhidi yake. Kwa muda mrefu Zuma amekuwa akitaja kuhusishwa na kashfa mbalimbali ambazo zingeweza kumuondoa madarakani na bila ya shaka ugumu wake wa kuamua kuondoka unatokana na uwezekano wa yeye kushtakiwa hivyo bila ya shaka anataka kupata uhakika wa usalama wake.

(124)

About the author

bongoz

1 Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • Kwanini wanafanya ufisadi wakiwa madarakani? Uongozi ni kitu kitukufu mno maana Mungu anahusika moja kwa moja linapokuja suala la kuongoza watu.Hivyo uadilifu si option,ndiyo sifa pekee ya kuwa kiongozi wa watu.

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available