KIMATAIFA TANZANIA

Nigeria: Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi Asimamishwa Kazi; Akutwa na Dola Milioni 43

  • Adai ni za kazi nyeti za kitengo
  • Makamu wa Rais apewa Jukumu la kuchunguza
  • Fedha taslimu zilihifadhiwa kwenye moja ya mahekalu yake
  • Bukhari aagiza ziingizwe benki kuu mara moja

Na. M. M. Mwanakijiji

LAGOS – NIGERIA (ZAMAMPYA) Mkurugenzi wa Taasisi ya Kijasusi ya Taifa ya Nigeria Balozi Ayodele Oke maarufu kama Ayo Oke – pamoja na Katibu wa Shirikisho la Nigeria Bw. Babachir Lawal wamesimamishwa kazi na Rais Mohammed Bukhari kufuatia tuhuma za ufujaji wa fedha za misaada ya kibinadamu pamoja na kukutwa na mabilioni ya Naira kwenye mojawapo ya majumba ya Taasisi ya Kijasusi  ya Taifa (National Intelligence Agency -NIA)

Siku chache zilizopita kufuatia udokezo kutoka kwa wasamaria wema maafisa kutoka Kamisheni ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi sawa na ile ya Tanzania ya Financial Crimes Unit walivamia jengo kubwa ambalo ndani yake walikuwa kiasi kikubwa cha fedha kilichofichwa kwa namna mbalimbali kiwemo kwenye kuta, nguo na sehemu nyingine zote zikiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 43 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 9.6.

Fedha zilizokamatwa Nigeria

Kufuatia kukamatwa kwa fedha hizo Mkurugenzi huyo alijitetea kuwa fedha hizo ni mali ya Idara ya Usalama wa Taifa kwa ajili ya operesheni nyeti ambazo zinahusiana na masuala ya usalama wa taifa. Hata hivyo, wakuu wengine wa idara hiyo walikuwa hawana taarifa na hata Rais Bukhari mwenyewe alikuwa hajui uwepo wa mpango huo. Hata hivyo Bw. Oke alidai kuwa fedha hizo ziliidhinishwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Goodluck Jonathan aliyeangushwa na Bw. Bukhari katika uchaguzi  uliopita.

Kitengo cha Uhalifu wa Uchumi na Fedha kilipoanza kufuatilia taarifa za uwepo wa fedha hizo kilijikuta kinakika kwenye anuani ya mtaa wa Osborne kwenye mji mdogo wa Ikoyi, jiji la Lagos ambapo waliingia kwenye ghorofa namba 7B. Uchunguzi umeonesha kuwa jengo  hilo lilikuwa linamilikiwa na kampuni ya Chobe Ventures Limited ambayo inadaiwa kumilikiwa na Bi. Folashade Oke, mke wa Mkurugenzi wa NIA.

Hata hivyo katika kujitetea kwake Mkurugenzi huyo amedai kuwa yote hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuhakikisha kuwa mali hiyo inakuwa salama na mke wake alikuwa ni mtu wa kuaminika zaidi na hivyo kuondoa hatari ya siri za mipango hiyo kuangukia kwa watu wabaya.

Hata hivyo, vyanzo vingine vya habari vinadai kuwa fedha hizo ni mabaki ya fedha ambazo Goodluck Jonathan alitumia katika kujaribu kununua viongozi mbalimbali wakati wa uchaguzi. Inadaiwa kuwa kuelekea uchaguzi wa 2015 Jonathan aliruhusu kutolewa kwa zaidi ya dola milioni 289 kutoka mojawapo kampuni tanzu za kampuni ya mafuta ya Nigeria kwenda Idara ya Usalama wa Taifa. Vyombo vya habari vyenye mrengo wa upinzani vimedai kuwa fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kununua uchaguzi na yumkini kiasi kilichokutwa kwenye nyumba ya Oke ni mabaki ya fedha hizo.

Kufuatia hili Bukhari amemuagiza makamu wake Bw. Yemi Osinbajo pamoja na mshauri wa masuala ya usalama na Mwanasheria Mkuu kufanya uchunguzi wa viongozi hao wawili na kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Wachunguzi wa mambo wanahofia kuwa endapo suala hili litaangaliwa kwa kina siri kubwa ya ufisadi inaweza kuibuliwa na kuitikisa taasisi  hiyo na hata kuweza kusababisha ifumuliwe.

Tayari timu hiyo imeanza kazi jana na kuwahoji wakuu wa idara mbalimbali akiwemo IGP wa Nigeria, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DSS – ambayo ni sawa na TISS ya Tanzania) na

Hata hivyo, siyo wote wanafurahia hatua hizi na hasa watu kutoka upinzani. Chama cha Upinzani cha PDP kimekejeli hatua hizi kwa kudai kuwa watendaji hao wawili walitakiwa wawe wametiwa pingu na kusaidia uchunguzi wakiwa jela badala ya kuundiwe tume kwa tuhuma nzito ambazo kama zingehusu viongozi wa upinzani bila ya shaka wangekuwa wameshatiwa ndani siku nyingi.

“Hatujafurahia uamuzi wa Rais Bukhari kuwachunguza watu hawa wakati tayari alishakubali ripoti iliyomsafisha Lawal mwezi Januari kwa tuhuma hizi hizi. Njia pekee ni kuhakikisha kuwa uchunguzi wa watu huru na wasio na upande na wanaoheshimika badala ya kuiacha serikali ijichunguze yenyewe” imesema taarifa ya chama hicho.

Wakati uchunguzi ukiendelea Rais Bukhari ameagiza kiasi chote cha fedha kirejeshwe Benki Kuu mara moja na kama ni fedha zinazotakiwa kwenda kwenye taasisi yoyote basi utaratibu mwingine utatumika kuzipata.

(187)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

Waandishi Makala

No recent posts available