Habari Kuu

Live: Taarifa Kuhusiana na Mtandao wa JamiiForums

Tunaweka mada hii hapa “Live”; kama kuna mtu yeyote ana update ya jambo lolote lile linaloendelea unaweza kutuma hapa moja kwa moja kupitia email ya mwanakijiji@jamiiforums.com  au unaweza kuweka maoni yako chini na tutakiposti kitu hicho chini ya mada hii: MMM

Mwandishi Maalum

Mtandao maarufu wa kijamii wa JamiiForums uko katika hali ya kuhimili mashambulizi ya kuzuia huduma na hivyo kukosesha wanachama na watembeleaji wake kusoma mtandao huo online. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, watu wanaojaribu kutembelea mtandao huo watakutana na taarifa za kuwa mtandao huo ni vigumu kupatikana kwa sasa hivi.

Mashambulizi ya kuzuia huduma – Distributed Denial of Service (DDOS) – hufanywa na watu au taasisi ili kuhakikisha kuwa tovuti fulani haipatikani. Namna mojawapo ushambuliaji huu unafanyika ni kwa kutumia computer ili kufanya mtandao uonekane unatembelewa na watu wengi kiasi cha kushindwa kuhimili watu wengi na hivyo kuzimika.

Uongozi wa JF umetoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa uongozi wake unajitahidi kurekebisha kinachoendelea. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, kutokana na shambulizi hili mtandao wa JF unaweza kukosekana mara kwa mara hadi hali itakapotengemaa. Wanachama na wageni wasicha kuangalia mara kwa mara.

(895)

bongoz April 26, 20182:48 am

Kutoka Dar nanTabora taarifa zinasema maandamano ya Mange yanapata shidabkuanza kwani waandamanaji hawajuani na hakuna aliye wa kwanza kunyanyua mabango. Polisi nao wanapata shida yabkutambua nani yupo kwa ajili ya maandamano na nani yupo katika shughuli zake…

bongoz April 26, 20182:17 am

Hadi hivi sasa hakuna sehemu yoyote ambayo imeripotiwa kuanza kwa maandamano au vijana kujitokeza kuunga mkono. Shughuli za sherehe za Muungano zinatarajia kuanza wakati wowote mjini Dodoma.

bongoz April 26, 201812:26 am

Bado mtandao wa JamiiForums unapata shida na wapo ambao wanaweza kuingia kwa kutumia VPN na wengine bado wanapata shida

About the author

bongoz

1 Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • Ndiyo shida ya matumizi ya domains za ndani. Uhuru wa upatikanaji wa habari kwa uharaka zaidi upo matatani sasa.

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available