Afya & Mazingira MAKALA

MAKALA; Mabadiliko ya Mara kwa Mara Chumba cha Kulala Uboresha Afya Yako.

Na DADA DOTTO

Chumba  cha kulala ni sehemu muhimu kuliko mahali popote katika nyumba. Tulio wengi huona sehemu hii kama mahali pa kupumzika pale tunapokuwa tumechoka na wakati wa kulala ndipo huwa tunakumbuka eneo hili.

Wakati mwingine tunajikuta tunapaacha chumbani tunapolala pachafu hatutandiki hata kitanda,huo ni uchafu. Fahamu kuwa hamna sehemu iliyo na maana sana katika maisha yetu kama chumbani au sehemu ya kulala.

Sehemu hii inapaswa kuwa tulivu, safi na yenye vitu  vichache, Unapoweka vitu vichache ndani ya chumba chako utakifanya kiwe na  hewa nzuri nzuri zaidi.

Chumbani  ni mahali ambapo unaweza kupumzisha ubongo wako na kufikiria mikakati   ya kimaendeleo na ukaweza kupata wazo jipya lakini yote hayo utayapata endapo chumba chako kitakuwa kisafi, tulivu pamoja hewa nzuri.

Kwa mujibu wa mtaalamu mmoja wa masuala ya saikolojia ,chumba kikiwa safi humfanya mtu awe huru na afya njema tofauti na mtu anaishi chumba kichafu mara nyingi kukumbwa na maradhi hali takayomfanya awe mnyonge.

Jinsi ya kukipendezesha chumba chako:

Mwanga

Chumba kinapopata  mwanga wakutosha huvutia zaidi  na kuwa na hewa ya kutosha. Hakikisha unakipa mwanga chumba chako na kukiacha kikiwa safi wakati wote ili kurahisisha hewa kuingia.

Mwanga wa taa za chumbani hauhitajiki wakati wa mchana jaribu kuwa makini kuzima taa mara unapoamka asubuhi na kuacha mwanga wa asili kutoka nje uingie chumbani kupitia dirishani.

Wakati wa usiku tumia taa makini za chumbani zenye mwanga wa kawaida ili usiumize macho taa ambazo uwekaji wake upo tafauti kulingana na uwezo ulio nao.

Kuna aina nyingi za taa ambazo huwekwa chini, ukutani au zile ambazo huwa pembezoni mwa kitanda. Mwanga wa taa ya chumbani hupaswa kuwa hafifu.

Rangi za chumbani.

Katika uchaguzi wa rangi ni pamoja na rangi ya ukuta wa chumba chako, mapazia, shuka, pamoja na rangi za mito. Hapa inategemea unapendelea rangi gani lakini unashauriwa rangi za chumbani ziwe rangi ambazo ni tulivu.

Hakikisha unabadilisha rangi ya chumba chako mara kwa mara kadiri ya uwezo wako itasaidia pia kukusahaulisha kipindi kigumu ulichowahi kupitia wakati ukitumia chumba hicho.

Sehemu ya joto utatakiwa kuweka mapazia ambayo sio mazito, katika hali ya baridi tumia mapazia mazito pia ni muhimu kuzingatia rangi, usipendelee rangi zitakazofanya chumba chako kuwa giza.

Pendelea mashuka yenye rangi moja au yenye maua machache. unapaswa kutumia rangi ambazo huonyesha usafi mfano rangi nyeupe.

Unaweza kuchanganya na rangi zingine katika mito yako ya kitandani.Ubunifu katika utandikaji wa kitanda chako ni muhimu ili kiweze kukuvutia muda wote.

Sakafu

Kuna watu wanaopenda kutumia Mazulia (carpets) chumbani. Jaribu  kuchagua rangi nzuri aidha inayoendana na ukuta wako wa chumbani, ilikuleta muonekano mzuri pia unashauriwa kapeti lisiingie chini ya kitanda ili kukupa  urahisi wakati wa kufanya usafi.

Ni muhimu kusafisha zulia lako ili kuondoa vumbi na kuepuka kupata mafua. Pia ni vema kuwa na tabia ya kulitoa maramoja moja ili kuweza kusafisha sakafu yako na kuondoa harufu ya unyevunyevu  uliopo chini ya zulia.

Mwisho kabisa,zingatia kuweka vitu vichache vinavyohitajika chumbani na kuwa na mpangilio mzuri wa vitu ndani ya chumba chako. Pendelea kuweka magazeti na majarida mbalimbali ili kukusaidia kupunguza mawazo.

(428)

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available