MAISHA MAKALA

Ijumaa na Da’Dotto: Mapenzi Yanaumiza, Uchunge Moyo Wako

Na Dotto Kwilasa.

img_20160922_0903071MAPENZI ya mbali, bila shaka hili neno sio geni masikioni mwako, inawezekana umesikia kwa jirani au wewe mwenyewe una mpenzi au mwenza anayeishi mbali nawe kutokana na utafutaji wa riziki au yuko mbali nawe kikazi.

Usiogope wala usiamini maneno ya watu kuwa wapenzi wa mbali huwa hawadumu ,jitahidi kuitumia hiyo nafasi   kuendelea kuliboresha penzi lako na mwisho kutimiza ndoto zenu mlizojiwekea za aidha kuoana kwa wale ambao bado wapo wapo au kudumisha ndoa yenu kwa ninyi mliooana.

Yakufaa ukumbuke kuwa Katika hili kuna mambo mawili ya msingi ambayo nataka kuyazungumzia kutokana na uelewa niliojaaliwa na mwenyezi Mungu ili kuhakikisha uhusiano wenu hautetereki lengo kuu likiwa ni kuchochea maendeleo katika jamii,si unajua mtu mwenye mawazo ya mapenzi huwa hawezi kufanya kazi.

Kwanza kabisa , hakikisha humsaliti mpenzi wako. Ukitaka kufurahia mapenzi, lazima usiwe msaliti na ujaribu kujali hisia za wengine. Upo msemo usemao, ukimsaliti mpenzi wako ujue nawe utasalitiwa, sasa ili uepukane na hilo ni vyema ukajiwekea dhana ya uaminifu wewe kama wewe kwanza.

Ili uwe na uhakika wa hiki ninachokisema hebu jiulize mwenyewe kimoyo moyo; “Kwa nini nimsaliti mpenzi wangu? Nampenda sana na najua nikimsaliti hatajua, lakini na yeye akinisaliti je?” Tafakari maneno hayo kwa makini sana, naamini kuna kitu utajifunza.

Usaliti huumiza watu hali inayowapelekea kukata tama ya kuishi na wakati mwingine hupelekea kupoteza uhai wao ,tafadhali epuka kusaliti uwape wengine furaha ya maisha yao ya kila siku.

Jichunge mwenyewe na kuchunguza kwa wengine maumivu ya kusalitiwa ili ufanye maamuzi sahihi, usikubali kabisa kuharibu thamani yako kwa kumruhusu mtu mwingine aujue mwili wako kwa kuwa tu umesikia ‘hamu’au tama ya mwili.

Jambo unalotakiwa kulithamini ni kukumbuka mwili wako ni kwa ajili ya mpenzi wako pekee, endelea na dhana hiyo siku zote utakazokuwa mbali naye, naamini utafurahi!

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili,baadhi ya wapenzi kusafiri sehemu moja hadi nyingine kwa lengo la kuwatembelea wenzi wao bila kujali ni mbali kiasi gani ili mradi tu kuporesha mampenzi kuepuka kuibiwa.

Hivyo basi,unapohisi una hamu ya kimwili kuliko kusaliti ni bora ukasafiri kwa ajili hiyo,hali hiyo itakusaidia kuwachukia wale wote wanaokushawishi kuumiza watu wasohatia.

Kama wewe umeamua kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako kwa kutambua thamani yake, hata Mwenyezi Mungu aatakulindia mpenzi wako huko alipo kwa kumwepusha na vishawishi japo lazima ufahamu jambo moja, Mungu anaweza kukulindia mwenzi wako ikiwa naye anakupenda kwa dhati na ana nia ya kuishi na wewe hapo baadaye.

Baada ya kuhakikisha kwamba humsaliti, sasa ni wakati wako wa kuhakikisha unamwamini katika kiwango cha mwisho.Usimwoneshe mashaka sana na nyendo zake. Wakati mwingine unaweza kumpigia simu asipokee, hilo lisikuchanganye.

Lakini pia ili kumwamini zaidi,kuna wakati unaweza kumpigia simu akapokea mwanamke,kilo pia lisikuchanganye kiasi cha kuchukua maamuzi magumu ya kushindwa kumwamini na kulipiza kisasi,inawezekana Yule aliepokea ni msaidizi wake au mazingira yalilazimu hali hiyo itokee.

Kuna baadhi ya watu, akimpigia simu mpenzi wake akiona hajapokea, tayari hisia zake zinakuwa mbali na muda huo huo anamwandikia meseji mbaya za ukali na kumtuhumu kwamba anajua huko aliko anamsaliti! Huna haja ya kufanya hivyo, onyesha kumwamini kama wewe ni mwaminifu yeye pia hana sababu za kukusaliti.

Kama umempigia na simu yake haipatikani, ni wakati wako wa kumwandikia meseji ya kumpa pole kwa kazi kutokana na kutambua kwako kwamba muda huo alikuwa bize ,inawezekana hapatikani kwa sabubu simu haina chaji au yupo katika wakati mgumu,hupaswi huchukua maamuzi ya kupayuka,jifunze kuonesha hisia juu yake.

Badala ya kumtumia meseji za matusi Jifunze kumkumbusha kuwa UNAMPENDA na kumthamini Ujumbe huo utamfurahisha na kumkumbusha mlikotoka, hata kama alikuwa na nia ya kukusaliti, hawezi kufanya hivyo kwani atakuwa anaumia moyo kiasi cha kujiona mnafiki.

Kumuamini kwako kutamfanya aone ni jinsi gani ambavyo wewe mwenyewe unavyojiamini na usivyo na wazo la kumsaliti! Kwa nini yeye akufanyie hivyo? Lazima atabadilisha wazo lake.

Mambo hayo  mawili ni ya msingi ambayo unatakiwa kuyazingatia pale unapokuwa mbali na mpenzi wako. Kumbuka kuwa mbali na huyo uliyetokea kumpenda haiwezi kuwa sababu ya nyie kutengana hakikisha unang’ang’ania mpaka uone mwisho wake ,usiwe mtu wa kukata tamaa.

 

Wazungu wanasema “some time you have to sacrifice what you have inorder to achieve your goal ”ukiwa mtu wa kukata tamaa mda wote utajishangaa  utajikuta umekuwa na idadi kubwa ya watu ulokuwa nao kwenye mahusiano ,ukipiga hesabu za haraha haraka unaweza kujaza fuso ..

Mtatengana tu endapo hakuna mapenzi ya dhati kati yenu lakini kama mmependana kiukweli kutoka mioyoni mwenu, hata muwe mbali kwa muda mrefu kiasi gani, bado hakuna cha kuliua penzi lenu.

 

Hakikisha unakuwa bize na mambo ya msingi kwa family yako ili uepuke uchochezi wa kumsaliti mwenza wako,inauma unaposalitiwa hebu jifunze kutowaumiza wengine.

 

MWISHO.

(323)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available