BURUDANI MAKALA

Chika ‘Nancy’ Ike Muigizaji wa Kike Mwenye Mafanikio Lukuki.

Na Dotto Kwilasa.

Chika ‘Nancy’ Ike ni muigizaji wa kike wa Nigeria alizaliwa  November 8, 1985  ni CEO wa kampuni ya Fancy Nancy Collections .images

Ni balozi wa umoja wa mataifa wa kupinga unyanyasaji dhidi ya wakimbizi ambapo kupitia kuchukizwa na unyanyasaji huo alianzisha kampuni yake inayoitwa CHIKA IKE FOUNDATION (Help A Child).

Muigizaji huyu wa kike amekuwa akijipatia umaarufu kwa miaka mingi kutokana na uigizaji wake mahiri na kuutumia uhusika katika filamu ipasavyo ambapo mwaka  2005 alicheza filamu iliyompa umaarufu mara dufu ikiwa na jina la  Sweetlove and Bless the Child iliyoongozwa na  TChidi Chikere.

Filamu hiyo ilimpatia tuzo ya mwigizaji bora wa kike anaechipukia  ambapo mwaka 2009 alichaguliwa kupewa tuzo ya mwigizaji mwanamke anayejitolea kuwasaidia wengine  kukuza vipaji.

Mbali na kuwa na mafanikio katika fani ya uigizaji kutokana

na kujiamini kwake ,hofu inakuja pale anaposhindwa kuhimili maumivu ya mapenzi ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa  kimkataba mwaka 2006 na mumewe, lakini baada ya miaka miwili mambo yakabadilika kila mtu akachukua njia yake.

1544971_10151955794772572_182746594_n

Alikuwa anaonekana na makovu mara kwa mara lakini akawa anaficha na kutoiambia jamii kilichokuwa kinaendelea. Maji yalipozidi unga ikabidi aondoke mwenyewe kutunza heshima, ingawa marafiki zake walivujisha siri.

Kama unavyojua mapenzi hayana mwenyewe,mbali na kwamba Chika ameigiza filamu nyingi za mapenzi na kuonyesha ujasiri lakini alishindwa kuhimili vishindo vya penzi hili halisia.

Kutokana na upweke 2013 Chika alianzishwa mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji nyota wa Ghana Van Vicker na kusababisha ndoa ya muigizaji huyu kuingia matatani lakini baadae mambo yalienda sawa .

Filamu alizowahi kuigiza ni pamoja na Heart of a Fighter (2011), Dangerous Beauty (2009, Power of Beauty (2007),The Prince of My Heart (2007), Mirror of Beauty (2007), My Only Girl (2006), Wisdom of the Gods (2006) na Soul Engagement (2006).

(14)

About the author

10cjlow1992

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available