BURUDANI MWANAKIJIJI

Burudani: Mbuni kwanini Habuni?

MBUNI HABUNI?

Ya’raabi nipe kauli, niseme hili na lile,
Kauli isiyo kali, isiwe kama ya yule,
Niseme lililo kweli, la mbuni hawa na wale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mbuni wana ile hali, hali yao ile ile,
Ukiuliza maswali, jawabu ni lile lile,
Watakukata kauli, ukajikuta mpole,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mnyama yule mkali, kawafuata mbuni kule,
Na meno yake hatari, kaingia hadi mle,
Akagenda nyalinyali, wasishtuke mbuni wale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mbuni wakaona zali, wakajifiche kule,
Wakajibanza kwa mbali, wakimkimbia yule,
Wakatafuta mahali, asije yule awale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Walipopata mahali, wakafanya vile vile,
Mchangani wakisali, wakajichomeka pale,
Hawakuuficha mwili, eti yule asiwale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Swali langu ndilo hili, ninawauliza wale,
Mbuni wanazo akili, au akili zao ni zile,
Za kutokuficha mwili, kisa kichwa kiko kule,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Nimeuliza hili, nazifunga beti zile,
Nafunga zangu kauli, naendelea na yale,
Msiniite katili, kwa kukumbushia lile,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Nje ya Jiji la Detroit, MI (USA).

(69)

About the author

bongoz

Add Comment

Click here to post a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available