Sisi ni Nani?

Gazeti la ZAMA MPYA ni Gazeti Huru la kila wiki ambalo linaongozwa na maadili thabiti ya uandishi wa habari. Gazeti hili linamilikiwa na OZ Company Ltd na hutolewa kwa njia ya mtandao pamoja na nakala zinazopatikana sehemu mbalimbali ambapo magazeti yanauzwa.

Gazeti hili lilianzishwa kama sehemu ya mwitikio wa kisiasa katika historia ya taifa kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2015. Katika uchaguzi huo Watanzania walikuwa wanapewa uamuzi wa kuchagua aina ya mabadiliko wanayoyataka. Waanzilishi wa gazeti hili kwa umoja wao waliamua kuona kuwa mabadiliko wanayoyataka wao na kwa watoto wao ni zaidi ya mabadiliko ya mtu. Ni mabadiliko ambayo yangeleta nidhamu katika utumishi wa umma, uwajibikaji na ambayo yatamjali mnyonge wa Tanzania.

Ni kutokana na ukweli huu ndio wazo la gazeti la “Zama Mpya” lilipozaliwa. Tunaamini kuwa zama hizi ni zama mpya kwa sababu taifa liko katika muda wa kupokezana vizazi katika uongozi na kuwa uongozi uliopo sasa unawajibu mkubwa sana katika kuhakikisha mapokezano hayo yanaenda kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji.

Kutokana na dhana hii basi gazeti hili linaongozwa na nadharia ya kimaadili ambayo inatutofautisha sisi na chombo kingine chochote cha habari. Ukitaka kujua zaidi kuhusu dhima na kanuni zinazotuongoza kimaadili TAFADHALI BONYEZA HAPA.

Utawala

Zama Mpya

Gazeti linalomikiwa na kampuni ya OZ (T) Limited.

OZ TV MAGUFULI ADAI TZ TUNAWEZA!

Bofya kutazama zaidi...

VIDEO YA LEO

KILICHOPOSTIWA PUNDE

PAYPAL

KUNDI LA HABARI

KINACHOENDELEA SASA

Waandishi Makala

No recent posts available